Mwandishi wa habari Zhang Zhan amehukumiwa kifungo cha miaka minne kwa kuripoti mlipuko wa kwanza wa virusi vya Corona katika mji wa Wuhan. Hukumu hiyo imetolewa na mahakama ya Shanghai.
Mahakama ya Shanghai imechukua uamuzi kifungo cha miaka minee dhidi ya mwandishi wa habari Zhang Zhan baada ya kuangazia mlipuko wa kwanza wa virusi vya Corona, amesema mwanasheria wake.
Kwa mujibu wa mashataka yanayomkabili, alisafiri hadi Wuhan mwezi Februari kuripoti kuhusu mlipuko wa virusi bila kuzingatia kanuni zilizowekwa.
Ripoti yake aliyoweka mubashara katika mtandao wa kijamii ilivuma sana mwezi Februari, ilimweka mashakani baada ya kuvutia mamlaka za China.
Kesi yake, ambayo imefunguliwa Jumatatu hii, ilichukua saa chache kbala ya kutolewa uamuzi. Mwandishi huyo wa habari, mwenye umri wa miaka 37, alikamatwa mwezi Mei mwaka huu, akishumiwa "kuchochea vurugu" kwa kueneza "habari za uwongo".
0 comments:
Post a Comment