Aina mpya ya kirusi cha corona kinachoaminka kusambaa kwa kasi, imeripotiwa kwa mara ya kwanza nchini Marekani na Amerika ya Kusini
Aina hiyo mpya ya kirusi cha corona kilichogunduliwa kwa mara ya kwanza nchini Uingereza, sasa kimeripotiwa kuingia Marekani katika mji wa Colorado.
Aina hiyo mpya ya kirusi cha corona kilichogunduliwa kwa mara ya kwanza nchini Uingereza, sasa kimeripotiwa kuingia Marekani katika mji wa Colorado.
Kirusi hicho kimegundulika kwa kijana wa miaka 20 ambaye hana historia ya kusafri.
Taarifa za vyombo vya habari za ndani zinasema kuna uwezekano wa kisa kingine cha kirusi hicho.
Wataalamu wanaamini kwamba aina hiyo mpya inaweza kuenea kwa kasi na itakuwa chanzo cha ongezeko la maambukizi Uingereza.
Aina hiyo mpya ya kirusi kinachujulikana kama B.1.1.7 tayari pia imeripotiwa Canada, Italia, India na Umoja wa Falme za Kiarabu. Chile nayo imeripoti aina hiyo mpya na kulifanya kuwa taifa la kwanza Amerika ya Kusini kubaini maambukizi yake.
0 comments:
Post a Comment