Sunday, 27 December 2020

SERIKALI KUGHARAMIA MAZISHI YA WALIOANGUKIWA NA JUMBA LA MAAJABU ZANZIBAR

...


Serikali imeahidi kugharamia mazishi ya watu wawili waliofariki baada ya kudondokewa na jen-go maarufu la kitalii, Beit Al Ajaib (Jumba la Maajabu) lililopo eneo la Mji Mkongwe mjini Unguja visiwani Zanzibar.

Waliofariki ni Pande Haji Makame (39) na Burhani Ameir Makuno (34) walibainika kati ya saa sita na saa nane usiku kwenye jitihada za kuwatafuta waliofunikwa na kifusi cha jengo hilo.

Wakati wawili hao wakitolewa katika kifusi, wengine wanne walikuwa wakitibiwa majereha waliyoyapata katika Hospitali ya Mnazi Mmoja.

Jumba hilo maarufu lililodumu kwa zaidi ya miaka 130 lilidondoka juzi mchana na kuwafunika mafundi waliokuwa wakilikarabati.

Jana Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla akifuatana na mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya aliwatembelea majeruhi waliolazwa na kwenda eneo la tukio

Katika hatua nyingine, Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama kufanya uchunguzi wa haraka ili kubaini chanzo cha kuporomoka kwa sehemu ya jengo la makumbusho la Taifa la Beit al Ajab.

Dk Mwinyi ametoa agizo hilo jana alipotembelea Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja ili kutoa rambirambi kwa wafiwa na kuwapa pole majeruhi wa ajali hiyo.

Amevitaka vyombo hivyo kufanya uchunguzi wa kina haraka ili kubaini chanzo cha kuporomoka kwa jengo hilo na kuleta maafa kwa wananchi ili Serikali ichukue hatua mara moja.



Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger