Wednesday, 2 December 2020

AIRTEL YAJA NA OFA YA SIKUKUU WATEJA KUPEWA DABO DATA

...

Mkuu wa Kitengo cha Data kampuni ya Simu za mkononi, Airtel, (kulia) na Meneja Mawasiliano wa Kampuni hiyo, Jackson Mbando wakizindua rasmi Ofa ya Siukuu kwa wateja kwa kuwapa Dabo Data. 
**
· Wateja wa Airtel Smartphone kupata Dabo Data kwa Nusu Mwaka. 

Kampuni ya simu za Mkononi Airtel Tanzania leo imetangaza kuzindua ofa ya Airtel Smartphone Dabo Data kwa wateja wote wa simu aina ya Smartphone kwa msimu huu wa sikukuu. 

Pia ofa hii itawanufaisha Wateja wote wa sasa wa Airtel wanyempango wa kubadilisha simu au Smartphone mpya kwa kujipatia Dabo Data kwa bando za wiki na mwezi kwa miezi sita ijayo yaani nusu mwaka. 

Airtel inapozindua Ofa hii ya shamrashamra za mwisho wa Mwaka Wateja wengine wa smartphone kwa sasa wanaweza kujiunga na mtandao wa Airtel ili kufurahi ofa hii. Ofa hii ni pale mtu mtumiaji wa simu aina ya smartphone anapotumia mtandao wa Airtel kwa mara ya kwanza kwenye simu yake. Ofa hii inatoa fursa kwa wateja kufurahia huduma yenye kasi ya Airtel 4G inayopatikana nchini kote Tanzania. 

Ofa ya Dobo Data inampa mteja mara mbili kwa kila bando analonunua ikiwa ni ya wiki au mwezi kwa kipindi cha miezi sita yaani Nusu Mwak. Ili kujipatia ofa hii, mteja wa smartphone anatakiwa kupiga *149*99#, changua 5 (intaneti) kisha 6 (Smartphone ofa) ili kujiunga. Baada ya kujiunga kikamilifu, mteja atapata ofa mara mbili ya bando lolote atakalo nunua iwe ni kwa siku saba au mwezi kwa miezi sita ijayo kuanzia siku ambayo amejiunga. 

Muda wa ukomo wa Airtel Smartphone Dabo Data ni sawa na ule ambao bando imenunuliwa na bonasi ya data kwa wale tu waliojiunga na ofa hii. 

Ezekiel Kahatano, Mkuu wa kitengo cha Data na Masoko Airtel Tanzania anasema, “Dhamira yetu siku zote ni kuwapa wateja wetu huduma bora ambayo inaendana na Maisha ya sasa ya kidigitali. Kwa maana hiyo, leo tunatangaza kuzindua ofa ya Airtel Smartphone Dabo Data, ambayo inawapa wateja unafuu kwenye kupata huduma bora ya Airtel 4G. Wakati tunakaribia msimu wa sikukuu, hii itawapa wateja wetu fursa ya kuendelea kuunganishwa na familia, marafiki na wadau wote kote nchini. 

Kwa upande wake, Meneja Mawasiliano Airtel Tanzania Jackson Mmbando anasema; 

“Ninachukua fursa hii kuwaomba wateja pamoja na watumiaji wa smartphone kujiunga na mtandao wa Airtel ili kufurahi ofa hii kwa WIKI na MWEZI kwa bando za intaneti kwa Nusu Mwaka. Tunaamini ya kwamba wakati wa kipindi hiki cha msimu wa sikukuu wateja wetu wanahitaji uhuru wa kuwasiliana na marafiki, familia na wafanya biashara wenzao na kwa hivyo huduma hii inawapa uhuru ule wanaohitaji”. 

Kuzindulia kwa ofa hii ya Smartphone data ambayo inampa bonua ya asilimia mia moja mteja inaonyesha ni kwa kiwango ngani tunavyothamini wateja wetu. Tuna Imani kuwa huduma hii itawapa hamasa wale ambao sio watumiaji wa smartphone kuanza kutumia na hivyo kukuza Maisha ya kidigitali kwa Watanzania.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger