Katibu wa UVCCM Wilaya ya Morogoro Manispaa bwana Hussein Egobano ambaye ndiye Mgeni rasmi kwenye mkutano huo wa ufunguzi wa Kampeni za Udiwani kata ya Magadu akiongea na watu waliofurika kusikiliza Sera za CCM.
Mgombea Ubunge Viti Maalumu Mkoa wa Morogoro Mhe. Dkt. Christine Ishengoma akizungumza kwenye uzinduzi huo wa kampeni kwenye kata ya Magadu a Manispaa ya Morogoro.
Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Morogoro Bi. Victoria Saduka akizungumza na wananchi wa Magadu wakati wa uzinduzi wa Kampeni hizo.
Mtia Nia Jimbo la Morogoro Mjini Bwana Salumu Mkolwe akizungumza kwenye a mkutano huo wa Ufunguzi wa Kampeni kata ya Magadu. Mgombea Udiwani Kata ya Magadu kwa TIketi ya CCM bwana Kiduka Juma Issa akijinadi mbele ya wananchi wa Magadu wakati wa uzinduzi huo wa Kampeni za Udiwani kwenye kata hiyo. Wananchi wa Kata ya Magadu na Viunga vyake wakisikiliza Sera na ahadi za viongozi na Mgombea wa CCM kata ya Magadu.
***************************************
Na: Calvin Edward Gwabara. Morogoro.
Mgombea Udiwani kata ya Magadu kupitia Chama cha Mapinduzi CCM bwana Kiduka Juma Issa amesema akipewa ridhaa kuwa muwakilishi wa wananchi wa kata hiyo atahakikisha anaiunganisha jamii hiyo na Chuo Kikuu Cha Sokoine cha Kilimo SUA ili kufaidi mambo makubwa yanayofanywa na watafiti wa Chuo hicho Borani Afrika.
Bwana Kiduka ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa Kampeni za Udiwani zilizofanyika kwwnye Mtaa wa Kididimo na kuhudhuriwa na mania ya wakazi wa kata hiyo ambayo imepata bahati ya kuwa na Chuo Kikuu Cha Sokoine cha Kilimo ambacho kinatoa mchango mkubwa kwa Taifa kwenye masuala ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.
“Kata yetu ina bahati ya kuzungukwa na wasomi wa SUA nitaunda Tume ya watu 7 ambao watakuwa wananishauri njia na mbinu njema za namna ya kata yetu kukutumia chuo kikuu hiki ili wana Magadu tuwe wa kwanza kuvuna na kunufaika na uwepo wa Chuo hiki cha pekeee nchini kwenye kata yetu” Alisema Bwana Kiduka.
Akizungumzia miradi mbalimbali ya maendeleo hasa changamoto ya maji kwenye kata ya Magadu Mgombea huyo amesema tayari Serikali ya magufuli imeshatoka Fedha kwaajili ya kujenga miundombinu ya maji ambayo tayari imeshaanza kujengwa na kwamba kukamilika kwake kutatua kero ya maji kabisa kwenye kata hiyo.
“ Naomba Mnitume kwenye Baraza la madiwani la Manispaa ya Morogoro nikawatumikie tuhakikishe za habari yetu ya kata ya Magadu ina öre she’s na kuanza kutoa huduma za kujifungua kwa wakina mama zetu ambao wanalazimika kwenda hospitali ya Mkoa na hospitali zingine kwa sasa, Sitaki uheshimiwa nataka niwe Mtumishi wa kweli” Alisisitiza Bwana Kiduka.
Pia ametumia nafasi hiyo kuomba kura kwa Mbunge, Mhe. Abdulaziz Mohamed Baood na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Joseph Magufuli kwa kusema kuwa tarehe 28 Octoba wachache Mafiga matatu yaani Rais, Mbunge na Diwani kutoka CCM wasisijeweka mafiga mawili ya Mawe na figa moja la Udongo ambalo muda wowote linaweza angusha Chungu.
Kwa upande wake Mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa Kampeni hizo za Udiwani kata ya Magadu Bwana Hussein Egobano ambaye ni katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini amesema amewataka wakazi wa kata ya Magadu wasifanye majaribio kama ambayo zilifanya kata mbili kwenye manispaa ya Morogoro kwa kuchagua upinzani maana miaka mitano yote hakuna walichofanya wapinzani hao.
Amesema Kata ya Magadu wenyeviti wake wa mitaa wote wanatoka CCM na Diwani ndiye mwwnyekiti wa Baraza la maendeleo ya Kata (BMK) hivyo wakichagua diwani wa upinzani watashindwa kuleta maendeleo maana wataishia kulumbana mambo ya siasa wakati wananchi wanataka maendeleo na hivyo kuwataka wamchague Kiduka Mgombea wa CCM awe Diwani wao walete maendeleo kwa haraka.
“Lakini pia ndugu zangu wa Magadu naleta salamu nyingi kutoka kwa Mgombea Ubunge wetu Mhe. Abood amefanya mambo makubwa ukitaka kujua yote angalia Kitabu cha kazi alizofanya katika kipindi cha miaka mitano yeye alikataa kuchukua hela za Gari kujinunulia gari akaamua kuzinunulia Gari la wagongwa (Ambulence) na sasa sote tunalitumia na magari mengine yanakuja Tumeogopa kuyaleta maana watasema anatoa rushwa ila akimaliza kuapishwa tu yatatoka” Alisema Bwana Egobano.
Aliongeza kuwa “ Tumpe kura za kishindo Rais John Pombe Magufuli maana amefanya mambo mengi kwenye Taifa letu na Manispaa ya Morogoro Nyinyi ni mashahidi angalieni Soko kubwa la Kisasa, Stand ya Mabasi ya Msamvu, Stendi ya Mabasi madogo ya kisasa na barabara za lami na mambo mengine mengi kwenye maji na afya, ili kumshukuru na kumtia moyo tumwagie kura za kishindo tarehe 28 Octoba.
Awali Mgombea Ubunge viti Maalumu Mhe. Dkt. Christine Ishengoma ambaye alikuwepo kwenye uzinduzi huo amewataka wakina Mama waache kudanganywa na Wapinzani kuwa watawapatia mikopo na kuchukua vitambulisho vyao vya Kupigia kura maana itawanyima haki yao ya msingi ya kupiga kura na mwisho wa siku Wagombea wa CCM wanaowataka watakosa kura zao.
“ Angalieni kazi kubwa iliyofanywa na Mhe. John Pombe Magufuli nchi nzima, niwaombe tujitokeze kwa wingi kupiga kura kuchagua wagombea wa CCM kwenye Udiwani, Ubunge na Urais kwa kishindo ili kata ya Magadu ndio iongoze Kitaifa kwa kuchagua kwa kura nyingi CCM na Wagombea wake” Alisema Dkt. Ishengoma.
Kwa upande wake akitoa salamu kwa niaba ya Watia nia wa Ubunge Jimbo la Morogoro Mjini na Mwenyekiti wa UVCCM Mstaafu Bwana Salumu Mkolwe amesema Kata ya Magadu imepata bahati sana ya kuwa na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo na ni fursa kubwa kiuchumi hasa kupitia walimu na wanafunzi wanasoma kwenye Chuo hicho.
“ Kuna miradi Mikubwa inatekelezwa na Rais John Pombe Magufuli kwenye chuo chetu cha SUA na miradi hii inaongeza idadi ya Wanafunzi wana jou ga na Chuo Hiki hivyo kuongezeka huko kwa wanafunzi jamii ya Magadu inanufaika kwa kuwapatia huduma mbalimbali za Vyakula, Malazi na mahitaji mengine na ukiangalia Wazee wetu huko mtaani kila mtu nyumbani kwake kapangisha Wanafunzi na hao wanafunzi wanalipa kodi Magadu inanufaika” Alisisitiza Mkolwe.
Uzinduzi huo wa kampeni kwa kata ya Magadu umeanza leo kwenye mtaa wa Kididimo na kutakuwa na Mikutano Mingine 6 kwenye kila Mtaa pamoja na kampeni za nyumba kwa nyumba kwa mujibu wa Mratibu wa Kampeni kata ya magadu Prof. Mombo ambaye alikuwa Mgombea Ubunge Viti maalumu Morogoro.
0 comments:
Post a Comment