Mgombea Ubunge wa Jimbo la Solwa Ahmed Salum akizungumza na wakazi wa Kata ya Didia Halmashauri ya Shinyanga wakati akifunga kampeni za uchaguzi.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa kampeni
Mkutano wa kampeni unaendelea
Na Marco Maduhu-Shinyanga
Mgombea ubunge Jimbo la Solwa (CCM) Ahmed Salum leo Oktoba 27,2020 amefunga kampeni zake katika Kata ya Didia na kuomba wananchi wampigie kura za ushindi ili awe mbunge wao na kuwaletea maendeleo.
Amesema tangu alipokuwa mbunge wa jimbo hilo mwaka 2005 hadi 2020, ametekeleza miradi mingi ya maendeleo, ikiwamo miradi ya maji, umeme, afya, pamoja na miundombinu ya barabara.
Aidha amesema siku ya kesho wananchi wa jimbo hilo wasifanye makosa, bali wampigie kura za ushindi ,pamoja na mgombea Urais John Magufuli na madiwani wote wa CCM, ili wawa letee maendeleo.
"Wananchi wa Didia na Jimbo lote la Solwa, kesho mkanipigie kura nyingi nishinde niwe mbunge wenu kwa awamu nyingine tena, ili nikamilishe miradi ambayo nimesalia kuikamilisha kwenye baadhi ya maeneo," amesema Salum.
"Nataka hadi kufika mwaka (2022-23) vijiji vyote vya Solwa 126, viwe na maji safi na salama, pamoja na umeme, na dhani mnafahamu kazi yangu mimi ni Mbunge wa vitendo," ameongeza.
Pia ameahidi kujenga vituo vya afya Didia na Lyabukande, kama alivyotekeleza Tinde , pamoja na Samaye.
Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Shinyanga vijijini Edward Ngelela, amewataka wananchi kesho wajitokeze kwa wingi kwenda kupiga kura ,ili watumie haki yao ya msingi kuchagua viongozi bora watakao waletea maendeleo, ambao wanatoka CCM.
0 comments:
Post a Comment