Saturday, 31 October 2020

AIRBUS AINA YA A220 -300' YENYE UWEZO WA KUBEBA ABIRIA 132 YATUA DODOMA KWA MARA YA KWANZA

...

 
Ndege aina ya Airbus A220-300 yenye uwezo wa kubeba abiria 132, ikitua kwa mara ya kwanza katika Uwanja wa ndege wa Dodoma baada kufanyiwa marekebisho kwa kupanuliwa kwa njia ya kutua na kufikia urefu wa kilometa 2.8.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt.Bilinithi Mahenge,akizungumza mara baada ya kuipokea  Ndege aina ya Airbus A220-300 yenye uwezo wa kubeba abiria 132,ambayo imetuwa kwa mara ya kwanza katika Uwanja wa ndege wa Dodoma baada kufanyiwa marekebisho kwa kupanuliwa kwa njia ya kutua na kufikia urefu wa kilometa 2.8.
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini(TANROAD), Mhandisi Patrick Mfugale,akitoa taarifa mara baada ya kuipokea Ndege aina ya Airbus A220-300 yenye uwezo wa kubeba abiria 132, ikituwa kwa mara ya kwanza katika Uwanja wa ndege wa Dodoma baada kufanyiwa marekebisho kwa kupanuliwa kwa njia ya kutua na kufikia urefu wa kilometa 2.8.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dk.Leonard Chamuriho,akizungumza mara baada ya kuipokea Ndege aina ya Airbus A220-300 yenye uwezo wa kubeba abiria 132, ikituwa kwa mara ya kwanza katika Uwanja wa ndege wa Dodoma baada kufanyiwa marekebisho kwa kupanuliwa kwa njia ya kutua na kufikia urefu wa kilometa 2.8.
Abiria wakishukwa kwa mara ya kwanza wakiwa na Ndege aina ya Airbus A220-300 yenye uwezo wa kubeba abiria 132,baada ya kutua katika Uwanja wa ndege wa Dodoma.
Baadhi ya wakazi wa Dodoma wakishuhudia Ndege aina ya Airbus A220-300 yenye uwezo wa kubeba abiria 132, ikituwa kwa mara ya kwanza katika Uwanja wa ndege wa Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt.Bilinithi Mahenge akiwa katika picha mbalimbali mara baada ya kuipokea Ndege aina ya Airbus A220-300 yenye uwezo wa kubeba abiria 132 baada ya kutua kwa mara ya kwanza katika uwanja wa Dodoma
…………………………………

Na Alex Sonna,Dodoma

Mambo yamezidi kunoga huku shangwe na mafuriko ya wakazi wa Dodoma baada ya kuiona Ndege aina ya Airbus A220-300 yenye uwezo wa kubeba abiria 132,kwa mara ya kwanza ikituwa katika Uwanja wa ndege wa Dodoma baada kufanyiwa marekebisho makubwa kwa kupanuliwa kwa njia ya kutua na kufikia urefu wa kilometa 2.8.

Ndege hiyo imetua jijini Dodoma na kupokelewa na viongozi mbalimbali,wananchi huku wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt.Bilinithi Mahenge.

Baada ya kupokea ndege hiyo, Dk.Mahenge amesema kuwa kutua kwa ndege hiyo inatokkana na Juhudi za Rais Dkt.John Magufuli kwa kuleta maendeleo kwa watanzania ili kurahisisha huduma za usafiri wa anga.

Hivyo Serikali imeamua kuboresha miundombinu ya huduma za usafiri wa ndege katika jiji la Dodoma ambao utawasaidia wakazi wa Dodoma kuachana na gharama kubwa za usafiri walizokuwa wakitumia awali kabla ya kuboreshwa kwa huduma za usafiri.

“Uwapo wa ndege hii ni mkubwa itakuwa inabeba abiria 132 kwani hapa zamani tulikuwa na ndege ambayo ilikuwa inabeba abiria 12 na bei yake ilikuwa ni Sh.530,000 wakati hii bei unaenda Dar es Salaam na kurudi ,”amesema Dkt.Mahenge

Kwa kweli nipende kusema kuwa kazi kubwa imefanywa na Rais Dkt,Magufuli kwa kuwajali watu wa kila aina kwa kuwaleta maendeleo kwa haraka lazima tumpongeze kwa hilo maana wana Dodoma ametushibisha tuendelee kumsaidia ili azidi kuing’arisha nchini yetu.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini(TANROAD), Mhandisi Patrick Mfugale, amesema kuwa uwanja huo awali ulikuwa na urefu wa kilometa 2.5 lakini kwasasa una kilometa 2.8 hivyo ndege zenye ukubwa wa ndege hii iliyotuwa zitakuwa zinatua jijini hapa.

Kwa upande wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dk.Leonard Chamuriho, amesema kuwa uwanja huo ulipanuliwa kwa awamu mbili ya kwanza ilikuwa kutua kwa ndege ya Bombadier yenye uwezo wa kubeba abiria 76 na hatua ya pili ni hatua ya kupanua ili ndege yenye uwezo wa kubeba abiria 132.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger