Wednesday, 28 October 2020

Watanzania Waanza Kupiga Kura Kuchagua Rais, Wabunge na Madiwani

...


Watanzania leo October 28, 2020 wameanza kupiga kura kuchagua Rais, wabunge na madiwani watakaoongoza kwa miaka mitano ijayo.

Hatua hiyo inakuja baada ya kumalizika kwa miezi miwili ya kampeni zilizovuta maelfu ya watu katika mikutano ya wagombea urais.

Lakini mikutano ya wagombea ubunge na udiwani ilivuta wananchi wachache na hivyo kuwalazimisha kutumia mbinu mbadala ya kujinadi, ambayo ilikuwa ni kuwafuata vijiweni, majumbani na katika sehemu zao za shughuli za kiuchumi.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (NEC), Jaji Semistocles Kaijage amesema katika uchaguzi, Tume itatumia jumla ya vituo vya kupiga Kura 81,567 vikiwemo vituo 80,155  vinavyotokana na daftari la NEC na vituo 1,412 vya ZEC.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger