Msanii wa BongoFleva na filamu, Video Vixen, Mjasiriamali Hamisa Mobetto amevunja ukimya kwa kusema yeye sio mtu wa kukata tamaa kwani anaamini kwenye ndoto zake na ukisikiliza watu wanavyosema hutofika.
Hamisa Mobetto amejibu hilo kwenye show ya Friday Night Live ya East Africa TV baada ya watu kumkosoa kwamba hawezi kuimba.
“Mimi ni mtu ambaye huwa sikati tamaa, huwa naamini katika ‘vision’ yangu mwenyewe, naamini ndoto zako ni za kwako ambazo umepewa na Mungu, kwenye haya maisha ukisikiliza watu wanachosema hutofika, kama ulipangiwa kufika sehemu fulani utafika tu hata kama iwe vipi” amesema Hamisa Mobetto
Aidha Hamisa Mobetto alizungumzia sababu za kuachana na meneja wake wa zamani Max Rioba ambapo amesema “Kwenye biashara na kazi kuna mikataba, kuna kazi na malengo pia, mimi na Max Rioba tuko poa kama kaka na rafiki. Kwenye maisha kila lenye mwanzo lina mwisho, kama unataka kupanuka zaidi, yeye ni muelewa na mimi pia hivyo maisha yanaendelea”
0 comments:
Post a Comment