Monday, 26 October 2020

Alichokisema Maalim Seif Hamad akifunga kampeni Zanzibar

...

 Chama cha ACT -Wazalendo kimehitimisha kampeni zake za Urais visiwani Zanzibar, ambapo mgombea urais kupitia chama hicho, Maalim Seif Hamad, ametoa tathimini juu ya kampeni zake alizozifanya visiwani humo. 

Akizungumza jana  katika viwanja vya Mnazi Mmoja Visiwani humo Maalim amewahimiza Wazanzabari kujitokeza siku ya kupiga kura kwa ajili ya kuwachagua viongozi wanaowahitaji.

“Tumefanya kampeni na kwa tathimini yangu ni nzuri tuliwaeleza dhamira zetu,ahadi zetu na nini mtegemee kutoka kwetu ikiwa nitakuwa Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi” Maalim Seif

“Mambo mengi tumesema kubwa kuboresha maisha kuhakikisha kila mzanzibari anapata ajira ,kuhakikisha vijana wetu wanapata elimu nzuri bila ya gharama mzazi” Maalim Seif



Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger