Monday, 26 October 2020

Alichokisema Hussein Mwinyi akifunga kampeni Zanzibar

...


 Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM, Dk Hussein Mwinyi amesema akipata ridhaa ya kuongoza ataboresha miundombinu ya umeme na kuwapunguzia gharama za nishati hiyo wananachi wasio na uwezo.

Dk Mwinyi alisema hayo jana kwenye mkutano wake wa kufunga kampeni uliofanyika uwanja wa Demokrasia, Kibandamaiti Unguja mjini.

Alisema dhamira yake ni kuifanya Zanzibar iwe na uchumi mpya ambao kwa namna yoyote utahitaji umeme wa kutosha.

“Nikichaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar nitahakikisha kunakuwa na vyanzo mbadala vya umeme vitakavyoendana na kasi ya viwanda na ukuzaji wa uchumi wa Zanzibar,” alisema.

Alivitaja vyanzo hivyo kuwa ni umeme wa jua, wa upepo na wa gesi asilia na kwamba watasambaza umeme katika vijiji zaidi ya 300 Unguja na Pemba.

Pamoja na hayo, alisema wataimarisha miundombinu ya umeme ya Pemba kutoka KV 11 hadi kufikia KV33 sambamba na kuimarisha Shirika la Umeme Zanzibar ( Zeco) kulitoa kutoka shirika linalojiendesha kwa hasara hadi kupata faida. Pia Dk Mwinyi aliahidi kujenga njia kubwa ya umeme ya msongo wa KV 132 kuelekea kusini na kaskazini mwa kisiwa cha Unguja yenye urefu wa kilomita 100 pamoja na kujenga vituo vikubwa viwili vya kupozea umeme.

Akizungumzia uimarishaji wa miundombinu ya bandari, alisema watajenga cherezo ili meli kubwa zifanyiwe matengenezo visiwani humo.

Kuhusu wakulima, Dk Mwinyi alisema atahakikisha wanapata elimu na utaalamu wa kilimo ili uzalishaji wao uwe na tija.



Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger