Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli amekiri kushangazwa na mambo Mungu anayoitendea Tanzania katiika kipindi hiki.
Rais Magufuli ameyasema hayo leo wakati akihutubia katika mapokezi ya ndege aina ya 'Air Bus' A220-300 leo, Disemba 23 jijini Dar es salaam.
Amesema kwamba kwa baraka ambazo Mungu amekuwa akiipatia Tanzania ni wazi haitashikika na kwamba mambo yataendelea kunyooka sana.
"Nataka niwahakikishie kadiri tunavyoendelea Tanzania haitashikika tutakuwa juu mno. Tanzania tunaweza na tutaweza. Mambo yananyooka mno mpaka mimi namshangaa Mungu. Mungu anatupenda na yupo pamoja na sisi", - amesema.
Pamoja na hayo, Rais Magufuli amesema kwamba 'Air Bus' ni ndege ya kwanza katika nchi za Afrika kutua Tanzania. "ndege hii ni ya kwanza Afrika hakuna nchi yoyote kuanzia North au South ambayo ina ndege kama hii na sisi tumepiga mbili kwa mpigo".
Mbali na hayo Rais amemuagiza mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege la ATCL kumpelekea majina ya watendaji wa Serikali 100 ambao wanakatiwa tiketi na Serikali lakini hawasafiri.
"Nimeambiwa kuwa baadhi ya tiketi huwa zinakatwa na watendaji wa serikali halafu hawasafiri kwahiyo nafasi ile inaenda tupu. Nimemwambia Mtendaji mkuu aniletee orodha ili tuwakate fedha hizo kwenye mishahara", -Rais Magufuli.
0 comments:
Post a Comment