Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amemkabidhi kiasi cha shilingi milioni 10, Mtanzania ambaye alisababisha Shirika la Ndege la Tanzania kuwa na ndege ya kwanza ambaye anafahamika kwa jina la Mapunda.
Rais Magufuli ametoa zawadi hiyo Jijini Dar es salaam wakati wa mapokezi ya ndege ya kwanza Afrika aina ya Air Bus A220-300 ambapo alimpongeza Mzee Mapunda kwa kuhatarisha maisha yake pindi alipokuwa angani akirejea Tanzania baada ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuvunjika ambao ndio walikuwa wamiliki wa ndege hizo.
Aidha katika mkutano huo Rais Magufuli alimuagiza Waziri wa Uchukuzi, Isaac Kamwelwe kuhakikisha Mapunda na mkewe wanasafiri bure kwenye ndege za ATCL katika safari zake zote.
"Kikubwa ninawaomba watanzania tuwe wazalendo, Mapunda asingekuwa mzalendo leo tusingekuwa na ndege, ninawaomba ATCL mumsafirishe bure mzee Mapunda kwa kazi kubwa aliyoifanya." amesema Rais Magufuli.
Ndege ya aina ya Air Bus A220-300 ni ndege ya kwanza kuwasili barani Afrika, hususani kwenye nchi ya Tanzania.
0 comments:
Post a Comment