Tuesday, 5 April 2016

Watu wawili wafariki kwa kuangukiwa na Kifusi Geita

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY


Watu wawili wamefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa vibaya huku mama mmoja Felista Mganga (65) akivunjika miguu yote baada ya kuangukiwa na kifusi wakati wakichimba mawe yanayodaiwa kuwa na dhahabu.

Tukio hilo limetokea juzi katika kijiji cha Busaka tarafa ya Nyamilembe Wilayani Chato Mkoani Geita wakati watu hao walipokuwa ndani ya mashimo hayo.

Wakizungumza na Channel Ten katika eneo hilo likiwa limefungwa kwa ajili ya usalama huku walinzi wakiwa wanalinda, baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wanaeleza jinsi hali ilivyokuwa.

Pamoja na ajali hiyo,wachimbaji hao wamepaza sauti zao na kuiomba Serikal kuwapatia maeneo salama zaidi ya kuchimba dhahabu kama ilivyoahidi wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka jana.

Kaimu Afisa Madini Mkoa wa Geita Fabiani Mshai amesema wachimbaji hao walivamia eneo hilo baada ya kuvumbuliwa na mchoma mkaa kuhu jeshi la Polisi Mkoa wa Geita likithibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Mwezi uliopita kijijini Mgusu Wilayani Geita watu wanane walifukiwa na kifusi huku watano wakipoteza maisha. 
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger