Saturday, 9 April 2016

MATOKEO MECHI YA YANGA VS ALHALY LEO TAREHE 9.4.2016 NI 1-1

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

YANGA imelazimishwa sare ya bao 1-1 katika mechi ya ligi ya Mabingwa wa Afrika dhidi ya Al Ahly ya Misri, mechi hiyo imechezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kwa matokeo hayo Yanga inahitaji nguvu za ziada ili kuweza kutinga hatua ya makundi kwenye michuano hiyo katika mechi ya marudiano itakayochezwa April 9 huko Misri.

Al Ahly ndo walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa mchezaji wao Amri Gamal baada ya mabeki wa Yanga kufanya madhambi na mwamuzi Dennis Dembele kutoka Ivory Coast kuamuru ipigwe faulo kuelekea lango la Yanga ikiwa ni dakika ya 11.

Dakika ya 19, Yanga walisawazisha bao hilo baada ya  Issoufou Boubacar kupewa pasi nzuri na Haji Mwinyi ambapo Issoufou alipiga mpira uliomkuta beki wa Al Ahly, Ahmed Hegazy ambaye alijifunga.

Dakika ya 34, Dembele alimpa kadi ya njano kipa wa Al Ahly kwa kuchelewesha mpira wakati Donald Ngoma akipiga shuti kali dakika 37 na kipa kudaka ikiwa ni pasi nzuri ya Juma Abdul.

Yanga ilifanya shambulizi kali kupitia kwa Salum Telela baada ya kupokea pasi ya Deus Kaseke hata hivyo shuti lake lilitoka nje huku Al Ahly wakikosa bao dakika ya 46 kupitia kwa Gamal ambaye mpira wake uligonga mwamba.

Mwamuzi Dembele aliendelea kutoa kadi za njano ambapo dakika ya 54 Telela alipewa kadi hiyo kwa kumchezea rafu Hassam Ghaly huku Thaban Kamusoko akikosa bao dakika ya 56 ikiwa ni pasi ya Kaseke.

Dakika ya 60, Kamusoko alimpa pasi nzuri Amissi Tambwe lakini alishindwa kufunga kwani tayari kipa wa Al Ahly aliuwahi na kuudaka huku kocha wa Yanga Hans Pluijm akifanya mabadiliko dakika ya 61 kwa kumtoa Issoufou nafasi yake ikichukuliwa na Geofrey Mwashiuya.

Ngoma alizidiwa ujanja dakika ya 66 na mabeki wa Al Ahly baada ya kumpora mpira akiwa anaelekea kuipatia Yanga bao la pili lakini mpira huo ukapigwa nje ya uwanja.

Pluijm alifanya mabadiliko mengine dakika ya 74 ambapo alimtoa Tambwe nafasi yake ilichukuliwa na Simon Msuva wakati Al Ahly nao waliwatoa Ramadhan Sobhi, Ghaly pamoja na Moaem Zakaria na kuwaingiza Walid Souliman, Housan Ashour na Malick Evouma.

Kipa wa Yanga, Ally Mustafa 'Berthez' alishindwa kuendelea na mchezo baada ya kuumia hivyo Deogratius Munishi 'Dida' alichukuwa nafasi yake ikiwa ni dakika ya 81 huku Ngoma akishindwa kufunga dakika ya 82 kwani shuti lake lilitoka nje ikiwa ni pasi ha Abdul.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger