za magari TZ.. watu wengi wamefariki na wengine kupata majeraha kutokana na ajali hizo.
Ripoti ya Jeshi la Polisi iliyotoka siku
chache zilizopita ilionesha kuwa Mwezi April 2015 umeongoza kwa kuwa
na ajali chache lakini idadi ya watu waliofariki ni kubwa zaidi tangu
mwaka 2015 uanze.
Naibu Waziri na Mbunge wa Bumbuli, January Makamba ameandika kwenye ukurasa wake wa
Ajali za barabarani
hazipaswi kuonekana kama jambo la kawaida.
Kusafiri kwa basi hakupaswi
kulinganishwa na kujitoa muhanga. APENDEKEZA;
1.Kuwe na taasisi mpya ya "Highway Patrol" yenye magari ya kutosha na
askari waadilifu. Traffic kuwa na vijiwe mahsusi barabarani haisaidii.
2.Magari ya abiria yawe na kifaa ambacho kinatoa mlio mkali ndani ya
basi spidi inapozidi na kutuma automatic SMS kwenye namba Maalum polisi
3. Highway Police wawe wanazunguka barabarani kila wakati badala ya kuwa na geti tu au kijiwe cha kupumzika.
4. Iwapo ajali itapatikana kutokana na ubovu wa basi, leseni ya kampuni
ya mabasi isimamishwe. Hii itawafanya wenye mabasi wawe makini.
5. Magari yanayoharibika barabarani hayapaswi kupaki highway siku tatu
yanapaswa kupewa masaa matatu kutengenezwa au kuondolewa barabarani.
6. Mamlaka ya usimamizi wa Usalama Barabarani kati ya SUMATRA na Polisi yabainishwe wazi ili kuwe na uwajibikaji.
7. Huduma za dharura za uokoaji wakati wa ajali, ikiwemo uwepo wa
helikopta, ni muhimu. Watu wengine hufa kwa kuvuja damu nyingi tu.
8. Ujenzi wa barabara, kwa maana ya upana wa barabara, mabega na
madaraja na alama na ishara za barabarani ni muhimu ukawa wa viwango.
9. Anapokamatwa dereva anayeendesha kwa uzembe, leseni yake isimamishwe
papo hapo. Akiwa amelewa asiruhusiwe kuendesha tena gari la abiria.
10. Ndani ya basi, au kwenye tiketi, kuwe na namba za simu za kupiga au
kutuma ujumbe Polisi abiria wakiona uendeshaji wa dereva hauridhishi
0 comments:
Post a Comment