Friday 15 March 2024

UJENZI WA DARAJA LA J.P MAGUFULI (KIGONGO-BUSISI) WAFIKIA 85%

...

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa akiwa na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu wakiwa wameshika bango linaloonesha maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Daraja la JP Magufuli (Kigongo - Busisi), lenye urefu wa kilometa 3 ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 85, Mkoani Mwanza.

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa akiwa na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu wakipokea maelezo kutoka Msimamzi wa mradi kutoka Wakala wa Barabara (TABROADS), Eng. Katelula Kasagwa, kuhusu maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Daraja la JP Magufuli (Kigongo - Busisi), lenye urefu wa kilometa 3, Mkoani Mwanza.

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa Daraja la JP Magufuli (Kigongo - Busisi), lenye urefu wa kilometa 3, Mkoani Mwanza.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Selemani Kakoso (Mb), akizungumza wakati Kamati hiyo ilipokagua maendeleo ya utekelezaji wa ujenzi wa Daraja la JP Magufuli (Kigongo - Busisi) lenye urefu wa kilometa 3, ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 85, Mkoani Mwanza.

Muonekano wa juu wa kazi za ujenzi wa Daraja la JP Magufuli (Kigongo - Busisi) lenye urefu wa kilometa 3 zikiendelea, Mkoani Mwanza. Ujenzi wa Daraja hilo umefikia asilimia 85.

..............

Ujenzi wa Daraja la J.P Magufuli (Kigongo - Busisi) lenye Kilometa 3.2 pamoja na Barabara unganishi ya Kilometa 1.66, linalojengwa kuunganisha Barabara Kuu ya Usagara - Sengerema - Geita katika Ziwa Victoria umefika asilimia 85 na unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Desemba, 2024.

Taarifa hiyo imetolewa Machi 15, 2024 Mkoani Mwanza katika ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu ikiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Selemani Kakoso (Mb) ilipoambatana na Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa kukagua maendeleo ya mradi huo.

Katika ziara hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Selemani Kakoso (Mb) ameeleza kuwa Kamati imeridhishwa na utekelezaji wa ujenzi wa daraja hilo na imempongeza Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha ili mradi huo ukamilike kwa muda uliopangwa.

Kakoso ameiagiza Wizara ya Ujenzi kuhakikisha anamsimamia Mkandarasi wa daraja hilo kutoa fedha zitakazokwenda kuisaidia jamii inayozunguka mradi huo ambazo zitakuwa kielelezo kwa wananchi wa Wilaya ya Sengerema na Misungwi.

Aidha, Kakoso ameitaka Wizara ya Ujenzi kuimarisha mifumo ya ulinzi na usalama katika daraja hilo ambalo linatokana na kodi za wanachi ili liweze kudumu kwa muda wa miaka 100.

Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amemshukuru Mhe. Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha ambapo mpaka sasa jumla ya Shilingi Bilioni 441.3 zimetolewa kwa ajili ya kumlipa Mkandarasi anayetekeleza mradi huo.

"Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anautazama sana mradi huu kipekee, amekuwa akitoa fedha kwa kila hati za Mkandarasi zinapowasilishwa na zimekuwa zikilipwa kwa wakati ili Mkandarasi asikwame kutokana na kukosekana kwa fedha", amesema Bashugwa.

Awali akitoa taarifa ya mradi, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Eng. Doroth Mtenga ameeleza kuwa mradi huo unatumika kama darasa la mafunzo kwa wanafunzi na wataalamu wetu wa ndani kupata uzoefu wa kusimamia na kujenga madaraja mengine kama hayo hapa nchini.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger