Mbunge wa Mkoa wa Mbeya Sophia mwakagenda kwa kushirikiana na wanawake wachimbaji wadogo wa madini wametoa msaada wa vitu mbalimbali vikiwamo 'diaper', sukari, sabuni na juice kwa akinamama waliojifungua na wanaosubiri kujifungua katika hospitali ya Wilaya ya Geita ikiwa ni Maadhimisho ya siku ya wanawake.
Akizungumza Mkoa Geita katika hospitali hiyo Mwakagenda alisema kuwa Kila mwanamke akijifungua lazima watu wamfariji huku akisema wao pamoja na wachimba hao wameona ni vema wakafariji akinamama hao na wale wanaosubiri kujifungua.
" Tunafahamu mwanamke yoyote anapojifungua lazima umpe pole, tumekuja hapa shopitali hii kuwapo hongera kwa waliojifungua na kuwatia moyo wale ambao wanaosubiri kujifungua kwa kuwapatia vitu kama sabuni,sukari "diaper"," ameeleza Mwakagenda.
Aidha alimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Geita Martin Shigela kwa kukubali ombi lake la kuungana na wanawake wachimbaji wadogo wa madini kwenda kutoa msaada huo na kufanya kongamano wachimbaji hao katika Mkoa huo.
Mbunge wa Mkoa huyo aliishukuru Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS),kwa kuwapatatia fedha kwa ajili ya kununua vifaa mbalimbali kwa ajili ya kutoa msaada kwa aiknamama hao.
Naye Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii kutoka Ofisi ya Takwimu ya Taifa(NBS),Ruth Minja amesema kuwa wameshirikiana na uongozi wa Mkoa wa Geita pamoja na mbunge huyo kutoa zawadi, msaada katika Hospitali hiyo kuonesha ushirikiano na wanawake ambao wapo hospitalini kama Jumuiya moja ya watanzania.
"Katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani ofisi ya NBS inashirikiana na wanawake wengine wote duniani pamoja na mbunge wa Mkoa Mwakagenda na uongozi wote wa Mkoa wa Geita tumefika hapa kwa ajili ya kuungana na wanawake wenzetu wachimbaji wadogo wanawake kuwapa faraja akinamama hawa,"amesema.
Kaimu Mkuu wa Mkoa huo Liliani Rwegoshora ameishukuru serikali kwa kuhakikisha wanawake wanafanya kazi katika mazingira bora huku akisema pamoja na kuwajali wanawake hao wameona ni vema wakatoa vifaa kwa akinamama waliojifungua na wanaosubiri kujifungua.
"Tunashukuru mbunge Mwakagenda pamoja na kampuni yake binafisi ya Shim Media ametokea Mkoa wa Mbeya kuja Geita kutuletea kongamano ambalo litatupatia elimu juu ya mambo mbalimbali kwa wanawake wachimbaji, tunajua serikali kazi yake kubwa ni kuhakikisha wananchi wanakuwa na afya njema na tukielekea katika kongamano la wiki ya wanawake," amesema.
Kwa upande wake Mganga Mfawidhi Hospitali ya Mji wa Geita Dk.Thomas Mafuru ametoa shukurani za dhati kwa wanawake wachimbaji wadogo wa madini katika Mkoa huo wakiongozwa na mbunge wa Mkoa wa Mbeya Mwakagenda katika siku ya Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani kwa kutoa faraja kwa wangonjwa ikiwa ni pamoja na msaada wa vitu mbalimbali.
Aidha Mganga Mfawidhi huyo ametoa rai kwa vikundi vya wanawake kwenda kutembelea Hospitali hiyo na kauwakaribisha kuwapatia faraja wagonjwa hospitalini hapo.
Mara baada ya kupokea zawadi hizo mmoja wa akinamama hao Ashura Jumanne amemshukuru mbunge huyo kwa kuwakumbuka kuwapafaraja ikiwa ni maadhimisho ya siku ya wanawake dunia.
0 comments:
Post a Comment