Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akiongoza kikao cha Kamati ya Ushauri Mkoa wa Shinyanga (RCC leo Alhamisi Machi 7,2024 katika ukumbi wa Chuo cha Walimu Shinyanga (Shycom). Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza wakati akifungua kikao cha Kamati ya Ushauri Mkoa wa Shinyanga (RCC) leo Alhamisi Machi 7,2024 katika ukumbi wa Chuo cha Walimu Shinyanga (Shycom).
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amewaagiza Maafisa Afya mkoani Shinyanga kuhakikisha sehemu zote zenye mikusanyiko ya watu kuwe na maji tiririka ya kunawa mikono na kuchukua hatua za kisheria pale watakapojiridhisha kuna mtu kwa maksudi hataki kufuata kanuni za afya na hivyo kusababisha ugonjwa wa kipindupindu kuendelea kusambaa.
Mhe. Mndeme ametoa agizo hilo leo Alhamisi Machi 7,2024 wakati akifungua kikao cha Kamati ya Ushauri Mkoa wa Shinyanga (RCC) kilichofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Walimu Shinyanga (Shycom) kikilenga kujadili mambo mbalimbali kuhusu Mkoa wa Shinyanga.
Mhe. Mndeme ugonjwa wa kipindupindu bado upo ndani ya Mkoa wa Shinyanga katika baadhi ya halmashauri ambapo mpaka sasa kati ya wagonjwa 216 walioripotiwa, wagonjwa 127 wamekutwa na vimelea vya kipindupindu hivyo kuagiza hatua madhubuti zichukuliwe ili kudhibiti kusambaa kwa ugonjwa wa kipindupindu.
"Halmashauri mbili zimeweza kuudhibiti ugonjwa wa kipindupindu ambazo ni Manispaa ya Kahama (siku 29 hawana mgonjwa) na Halmashauri ya Kishapu (siku 9 hawana mgonjwa). Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga imeendelea kupata wagonjwa kipindupindu baada ya kukaa kwa muda wa siku 13 bila wagonjwa (Februari 12- 25,2024. Na kwa Manispaa ya Shinyanga kata za Ndala na Kambarage zimeathirika zaidi",amesema Mhe. Mndeme.
Mkuu huyo wa Mkoa amesema pia bado mkoa wa Shinyanga unakabiliwa na changamoto ya kupanda kwa bei ya sukari hivyo amewaelekeza Mawakala wote wanaouza sukari ndani ya mkoa wa Shinyanga waendelee kuzingatia maelekezo ya serikali kwa kuuza sukari kwa bei elekezi ambapo bei ya rejareja ni kati ya shilingi 2,800/= hadi 3,000/= kwa kilo moja na kwa bei ya jumla ni kati ya shilingi 2,650/= hadi 2,800/= ambapo kwa mfuko wa kilo 50 ni kati ya shilingi 132,500/= na shilingi 140,000/=.
Mhe. Mndeme pia ameziagiza Halmashauri kutenga maeneo maalumu kwa ajili ya wafugaji ambayo hayataathiri shughuli za kilimo na utunzaji maliasili ili kuongeza uzalishaji wa ng'ombe, mbuzi na kondoo kutokana na kwamba Shinyanga kuna Machinjio ya kisasa huku akiwataka maafisa mifugo kutembelea wafugaji na kuwapa elimu ya ufugaji wa kisasa hali ambayo italeta mazingira rafiki kwa wafugaji waache kuhama mkoa kwenye kutafuta malisho.
Katika kikao hicho cha RCC, mbali na wajumbe kujadili masuala mbalimbali kuhusu maendeleo ya mkoa, pia taarifa mbalimbali zimewasilishwa ikiwemo taarifa ta Mpango na Bajeti ya Mkoa wa Shinyanga kwa mwaka wa fedha 2024/2025, taarifa ya mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu kwa Mkoa wa Shinyanga, taarifa ya sukari, taarifa ya sekta ya maji RUWASA, KASHWASA, KUWASA na SHUWASA, taarifa ya usambazaji wa huduma za umeme na taarifa ya sekta ya miundombinu (TANROADS na TARURA).
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza wakati akifungua kikao cha Kamati ya Ushauri Mkoa wa Shinyanga (RCC) leo Alhamisi Machi 7,2024 katika ukumbi wa Chuo cha Ualimu Shinyanga (Shycom). Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza wakati akifungua kikao cha Kamati ya Ushauri Mkoa wa Shinyanga (RCC) leo Alhamisi Machi 7,2024 katika ukumbi wa Chuo cha Ualimu Shinyanga (Shycom).
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza wakati akifungua kikao cha Kamati ya Ushauri Mkoa wa Shinyanga (RCC) leo Alhamisi Machi 7,2024 katika ukumbi wa Chuo cha Ualimu Shinyanga (Shycom).
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akiongoza kikao cha Kamati ya Ushauri Mkoa wa Shinyanga (RCC)
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akiongoza kikao cha Kamati ya Ushauri Mkoa wa Shinyanga (RCC
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Prof. Siza Tumbo akizungumza wakati wa kikao cha Kamati ya Ushauri Mkoa wa Shinyanga (RCC) leo Alhamisi Machi 7,2024 katika ukumbi wa Chuo cha Ualimu Shinyanga (Shycom).
0 comments:
Post a Comment