Wednesday, 27 March 2024

MIAKA MITATU YA RAIS SAMIA ,TANROAD TANGA YAJIVUNIA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO

...

 

Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (Tanroad) Mkoa wa Tanga Mhandisi Dastan Singano akizungumza na waandishi wa habari ambao hawapo pichani




Na Oscar Assenga, TANGA.

SERIKALI kupitia Wakala wa barabara nchini (Tanroad) Mkoani Tanga imetengewa Bilioni 294 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya barabara inayoendelea kwa sasa ikiwemo barabara ya Tanga-Pangani.

Hayo yalisemwa na Meneja wa Wakala wa Barabara Mkoani Tanga (Tanroad) Mhandisi Dastan Singano wakati akielezea miaka mitatu ya Rais Dkt Samia Suluhu ambapo alisema wanajivunia utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Ambapo alisema Serikali ya awamu ya sita imejikita kuleta Maendeleo ya Miundombinu ya barabara kwa Mkoa wa Tanga na katika barabara hizo kuna miradi inayoendelea.

Aliitaja miradi hiyo kuwa ni ule wa Barabara ya Tanga-Pangani ikiwemo Daraja la Mto Pangani mpaka Tungamaa kuelekea Mkwaja hadi Makange pamoja na Barabara ya Handeni-Mafleta.

Aidha alisema kwamba miradi hiyo inaendelea na utekelezaji wake na kwa sasa imefikia asilimia 73 vilevile Daraja la Pangani na barabara zake mradi inaendelea kutekelezwa kwa tija kubwa

“kwa kweli kwa kipindi cha miaka mitatu ya Rais Dkt Samia Suluhu sisi kama mkoa wa Tanga tunajivunia uwepo wa miradi mikubwa ya maendeleo ikiwemo mradi wa Tanga-Pangani-Daraja la Mto Pangani -Tungamaa kwenda Mkwaja mpaka Makange barabara inaedelea kutekelezwa”Alisema Meneja Singano.

Meneja huyo alisema pia kwa sasa wanaendelea na utekelezaji wa barabara ya Handeni –Mafleta iliyopo chini ya Mkandarasi huyo amepata kipande kingine cha Mafleta kwenda Kweleguru hata hivyo mradi kutoka kwaleguru utakwenda hadi Kibirashi mpaka kule mpakani mwa Manyara hiyo barabara mpaka Singida inatekelezwa kwa utaratibu huo na utaona miradi mikubwa inaendelewa.

Akizungumzia kuhsu namna walivyojipanga kukabiliana na uharibifu wa muondombinu hususani katika kipindi cha mvua alisema wamejipanga kukabiliana na changamoto za barabara na Bajeti ya matengenezo ni zaidi ya milioni 12.6 imetengwa .

“Lakini pale panapotokea dharura kuna fedha za dharura ambazo wanazitumia kwa ajili ya sehemu ambazo zimepata itilafu ya kukatika kwa barabara kwa lengo la kuondosha changamoto hizo”Alisema Mhandisi Singano.

Meneja huyo alisema kwa sasa matarajio yao ni kuanza mradi wa barabara ya Soni hadi Bumbuli mpaka funta wilayani Lushoto wenye kilomita 20 na wanandelea na upembuzi yakinifu na usanifu wa kina ikiwemo barabara ya Old Korogwe-Kwamkoro-Maramba mpaka Mabokweni.

Alisema barabara hiyo pia wanakamilisha usanifu ili iweze kujengwa kwa kiwango cha lami na wana mpango wa kujenga barabara kutoka njia ya panda kiomoni kwenda mpaka Bamba wilayani Mkinga kutokea Mlingano wilayani Muheza .

“Kwa hiyo utaona namna gani serikali ya awamu ya sita imejikita kuleta Maendeleo ya Miundombinu ya barabara kwa Mkoa wa Tanga zitakazokuwa na tija ya kuchochea kufungua maendeleo na kukuza uchumi”Alisema
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger