Tuesday, 15 August 2023

RAIS SAMIA AZINDUA JENGO LA SAFINA DODOMA

...





Na Dotto Kwilasa, DODOMA 

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dk.Samia Suluhu Hassan amezindua jengo la kitega uchumi la Kanisa la Angikana Central Dodoma (DCT) lililopewa jina la Safina House huku akiweka msimamo wake Katika kuimarisha amani na utulivu nchini.

Amesema Kutokana na utulivu uliopo,kamwe Taifa halitayumbishwa dhidi ya watu wasio itakia mema Tanzania na kutumia nafasi hiyo kuwaomba viongozi wa Dini kuendelea kuhubiri amani, umoja na mshikamano.


Akizindua jengo hilo la kitegauchumi Leo Agosti 15,2023 jijini hapa, DK.Samia amesema,"Niwasihi viongozi wote wa dini nchini kuendelea kuliweka Taifa letu  katika mikono salama ya mwenyezi mungu ili lidumu katika umoja, amani na mshikamano. Kamwe tusikubali kuyumbishwa na mtu yoyote yule asiyelitakia Taifa mema,”anasisitiza


Amesema serikali  inatambua mchango wa taasisi za kidini nchini ambapo zimekuwa zikisaidia katika kutoa huduma za kijamii  kwa wananchi ikiwemo elimu, kilimo na Afya.


Amefafanua kuwa Kabisa Angrikani ni kanisa kongwe zaidi duniani,na kwamba tangu kuingia kwake nchini limekuwa likitoa huduma kwa wananchi kwani shule nyingi zilijengwa ikiwemo shule ya msingi Mvumi,Mazengo na shule ya sekondari ya Msalato.


“Nimefurahi kusikia kuwa mnajihusisha na na kutoa mafunzo ya kilimo hasa Dodoma ambapo kuna ukame lengo ni kuhakikisha watu wanakuwa na chakula cha kutosha na salama kama ilvyonukuliwa katika kitabu cha zaburi ya 15;16,”


Aliongeza kuwa :“Suala la kilimo ni jukumu mlilobeba na ndio nguzo kuu ya serikali ndio maana tunatekeleza mradi wa Jenga Kesho Iliyobora (BBT) lengo ni kuhamasisha vijana kuingia katika kilimo, uvuvi na ufugaji.”


Katika hatua nyingine Dk.Samia alieleza kuwa  serikali itaendelea kuenzi mchango wa kanisa la Anglikana pamoja na kudumisha umoja na mshikamano na kuifikisha Tanzania pale inapotakiwa.


“Muendelee kuwaimiza watanzania  kufanya kazi kwa bidii na kuchangamkia fursa zilizopo Dodoma kwa ninyi ni mashaidi mtaona jiji hili linavyobadilika siku hadi siku  na mwakani tutaitana wana pamoja  kuelezana yote yaliyofanyika,”alifafanua


Kwa upande wake Askofu wa Dayosisi ya Central Tanganyika (DCT) Dk.Dickson Chilongani  alimpogeza Rais Dk.Samia kwa  kushiriki tukio hilo kwani  ujio wake unaonyesha kuwa yeye ni kiongozi wa Dini zote.


Alisema hiyo  sio mara ya kwanza kushiriki Rais Dk.Samia kushiriki katika matukio kama hayo.


“Sisi tunaendelea kukupongeza Rais Dk.Samia  kwa uongozi wako  mahili wako na kazi unazoendelea kuzifanya kwa maendeleo ya wananchi.Tangu umepokea kijiti hujayumba wala kuteteleka kwani miradi yote ya kimkakati iaendelea ikiwemo ujenzi wa bwawa la mwalimu nyeerere.


Ameongeza kuwa :”Miradi mingine ambayo inaendelea kutekelezwa ni ujenzi wa reli ya kisasa, barabara ya mzunguko, kukamilika kwa mji wa serikali, ujezi wa ikulu chamwio a ujenzi wa vituo vya afya a shule katika kila koa ya Tanzania hivyo uchumi kuendelea kukua.Tuamuomba mungu akujalie ili utuvushe hapa tulipo  utupeleka katika Tanzania mpya.


Dk.Chilongani amesema  DCT inaundwa na wilaya tatu za Dodoma ikiwemo Chamwino, Bahi na Mpwapwa ambapo kwa sasa  ina jumla ya waumini 700,000 na wachungaji 300  ambapo kati ya wachungaji hao 65 ni wanawake ambao wamehitimu ngazi mbalimbali za elimu.


 “Naishukuru serikali yako kwa kuendelea kutoa vifaa mbalimbali ikiwemo vitabu, walimu na chakula ambapo Hadi sasa DCT imefanikiwa kusomesha vijaa 7,000  wa shule za msigi a sekodari amapo wapo katika hatua mbalimbali za maendeleo.


Akizungumzia kuhusu jengo hilo Dk.Chilonga amesema  ujenzi wake ulianza  mwaka 2017 ambapo hadi kukamilika kwa jengo hilo wametumia sh.bilioni nane  ambapo kati ya hizo sh.bilioni mbili ni msaada kutoka kwa rafiki kutoka Newyork.


Kwa upande wake Askofu Mkuu wa Kanisa la Angrikana Tanzania Dk.Maimbo Mndolwa alisema kanisa hilo limekuwa likifanya kazi kwa kushirikiana na serikali.


“Leo umechukua nafasi ya kipekee kuungana nasi.kanisa linafanya kazi za kimaendeleo na kijamii  na tunafanya kazi na makundi mbalimbali ya watu wenye changamoto.”


Ameongeza kuwa :”Kanisa linaendelea  kuiombea serikali kwasababu hata Rais Dk.Samia anapigwa maneno mengi lakini watu hao ndio wa kwanza kula matunda ambayo yanatokana na uongozi wa serikali yake.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger