Diwani wa viti maalum,Ester Makune akizungumza na wachezaji wa timu mbili kwenye uzinduzi wa mashindano ya UVCCM FOOTBALL CUP 2023 kabla ya kuanza mtanange wa kwanza katika uwanja wa chuo cha ualimu Shy Com.
Na Halima Khoya,Shinyanga
Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Kata ya Mjini Manispaa ya Shinyanga (UVCCM) umezindua mashindano ya mpira wa miguu “UVCCM FOOTBALL CUP 2023” yanayohusisha timu nne za ya mpira wa miguu kwa kila mtaa katika kata hiyo ili kutafuta timu moja itakayokuwa timu ya Kata.
Mashindano hayo yamezinduliwa leo Agosti,17,2023 Katika uwanja wa chuo cha ualimu Shy Com na kuhitimishwa agosti,19,2023 ambapo itakua fainali kati ya timu iliyoshinda leo Town stars ya mtaa wa viwandani dhidi ya Stjoseph ya mtaa wa Kaunda na timu itakayoshinda kesho.
Akifungua mashindano hayo,Diwani wa viti maalum,Ester Makune amesema michezo kwa vijana ni tiba na huimarisha afya hivyo amewataka kucheza mpira wenye nidhamu na kuchukua kama faida mashindano hayo ili kutengeneza njia ya mafanikio.
Kwa upande wake,Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Mjini,Abdul aziz Said amesema mashidano hayo yatasaidia vijana kuepukana na makundi yasiyofaa (Vibaka,watiumiaji wa madawa ya kulevya) sambamba na kupunguza wimbi la vijana wasiokuwa na ajira mtaani.
“Kauli mbiu ya mashindano haya ni “Mpira ni ajira”,vijana mchukue nafasi hii kuonyesha vipaji vyenu,mpira unalipa mpira unaajiri,timu mbili za kwanza zimeshacheza na mshindi ni Town stars ambaye atacheza na mshindi wa kesho” amesema” Said.
Nae Mwenyekiti wa Mtaa Viwandani,Ashraf Majaliwa,amesema amefurahishwa na ushindi walioupata na kwamba ameupokea kwa furaha na kwamba wanamatumaini makubwa juu ya timu yao hivyo wanatarajia kushinda fainali.
Diwani wa viti maalum,Ester Makune akikagugua wachezaji wa timu mbili kwenye uzinduzi wa mashindano ya UVCCM FOOTBALL CUP 2023 kabla ya kuanza mtanange wa kwanza katika uwanja wa chuo cha ualimu Shy Com.
Viongozi wakifuatilia mpira wa miguu uliochezwa leo Agosti,17,2023 kwenye uwanja wa Shy Com majira ya saa 10 kati ya timu ya mtaa wa kaunda na viwandani.
Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Mjini,Abdul aziz Said akizungumza mara baada ya kumalizika mechi ya awamu ya kwanza iliyochezwa Agosti,17,2023 katika uwanja wa Shy Com Mkoani Shinyanga.
Mwenyekiti wa Mtaa Viwandani,Ashraf Majaliwa akizungumza mara baada ya kumalizika mechi ya awamu ya kwanza iliyochezwa Agosti,17,2023 katika uwanja wa Shy Com Mkoani Shinyanga ambapo ushindi umeenda katika Mtaa wake.
0 comments:
Post a Comment