Wednesday 30 August 2023

WAANDISHI WA HABARI SHINYANGA WATEMBELEA BANDARI ZA ZIWA VICTORIA NA BANDARI YA NCHI KAVU ISAKA

...
Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Agosti 30,2023 wametembelea Bandari zinazosimamiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kwa ajili ya kujionea na kujifunza namna zinazovyofanya kazi. 

Bandari walizotembelea ni pamoja na Bandari ya Nchi Kavu ya Isaka wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga pamoja na Bandari za Ziwa Victoria (Kusini na Kaskazini)

Wakitembelea bandari hizo waandishi wa habari wamejionea namna Serikali inavyowekeza kwa kufanya maboresho makubwa kwenye Bandari hizo na kuchochea ukuaji wa uchumi hapa nchini.

Meneja Bandari za Ziwa Victoria Frednand Nyathi, amesema katika maboresho ya Bandari tatu za Mwanza Kaskazini, Kemondo na Bukoba, Serikali imetenga kiasi cha fedha Sh. bilioni 60 kwa ajili ya kuzikarabati.

Amesema maboresho hayo yataongeza ufanisi wa utendaji kazi wa Bandari pamoja na kuongeza mapato na kukuza uchumi wa nchi.

Afisa Bandari ya Isaka wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Abel Mshana amesema Bandari hiyo Kavu imekuwa ikirahisisha utendaji wa bandari na imekuwa ikihudumia nchi tano kusafirisha mizigo ikiwemo Rwanda,Burundi,Uganda, Sudani Kusini na DRC.

Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoani Shinyanga (SPC) iliyoandaa ziara hiyo, Greyson Kakuru amesema katika ziara hiyo wamejifunza mambo mengi ya uwekezaji wa Bandari ambao ni kichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi hapa nchini ikiwemo maboresho makubwa ya bandari.

Meneja wa Bandari za Ziwa Victoria Ferdinand Nyathi akizungumza na waandishi wa habari

Afisa Bandari ya Nchi Kavu Isaka mkoa wa Shinyanga Abel Mshang'a akizungumza na waandishi wa habari

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive

Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger