Thursday 24 August 2023

MKUU WA WILAYA AWAHIMIZA WANA-BUSEGA KUTOA MAONI KWA UWAZI BEI ZA MAJI

...




Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Anna Joram Gidarya, amewataka wananchi wa Wilaya ya Busega kutoa maoni kwa uhuru kuhusu ombi la kurekebisha bei za maji na usafi wa mazingira kutoka Mamlaka ya Maji Busega wakati wa mkutano wa kutafuta maoni uliofanyika mjini Lamadi, Wilayani Busega, leo 24 Agosti 2023.

“Serikali imewaamini EWURA na kuwatuma hapa kupokea maoni yetu wana-Busega  ili tuweze kupata bei za huduma ya maji na kuilinda Mamlaka yetu isife, hivyo niwasihi sana mtoe maoni kwa uwazi na bila woga,” alisema. 

Mhe  Gidarya ameitaka EWURA kuendelea kuisimamia BUSEWASA kwa umakini, kwani Serikali inaamini katika utendaji mahiri wa mdhibiti  ili kuhakikisha huduma za maji bora zinaendelea kupatikana na kwa wananchi wa Busega.

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa EWURA katika mkutano huo, Bw. George Mhina ambaye pia Meneja wa EWURA Kanda ya Ziwa, alisema EWURA itaendelea kutekeleza wajibu wake kwa mujibu wa sheria.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Busega, Mha. Romanus Thomas, alieleza sababu za kuomba marekebisho ya  bei za maji ni kuongeza mtandao wa usambazaji huduma za majisafi na usafi wa mazingira, kuongezeka gharama za uendeshaji ikiwamo gharama  za umeme na gharama za kutibu maji.

Mwisho.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger