Thursday 17 August 2023

MKOA WA TANGA UNA CHANGAMOTO KUBWA YA MATUKIO YA AJALI ZA BARABARANI HUSUSANI ZA WANAFUNZI

...
 Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoani Tanga (RTO) Wiliam Mwamasika akizungumza wakati kuelezea mpango kazi wa Usalama barabara kwa Jiji la Tanga unaendeshwa na Shirika la Amend Tanzania ambao umefikia asilimia 90.
Meneja wa Shirika la Amend Tanzania Simon Kalolo akielezea  Mpango Kazi wa Usalama Barabarani
Mmoja wa madereva waliokiuka sheria za usalama barabara Avishai kushoto akiandika maelezo ya kutokurudia kosa la kutokusimama kwenye kivuko cha waenda kwa miguu baada ya kukamatwa kwa kosa hilo leo na kufikishwa kwenye mahakama ya watoto iliyokuwa ikishikiliza kesi za madereva waliovunja sheria za barabarani kulia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani mkoa wa Tanga William Mwamasika
Mahakama ikiendelea
Elimu ikitolewa kwa waendesha bodaboda

Wanafunzi wakifiatilia mahakama hiyo





Na Oscar Assenga,TANGA

JESHI la Kitengo cha Usalama barabarani mkoani Tanga limesema kwamba mkoa huo una changamoto kubwa ya matukio ya ajali hususani kwa watoto na wanafunzi wanapotoka majumbani kwenda shuleni na wanaporejea.

Hayo yalibainishwa leo na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoani Tanga (RTO) Wiliam Mwamasika wakati wa kuelezea mpango kazi wa Usalama barabara kwa Jiji la Tanga unaendeshwa na Shirika la Amend Tanzania ambao umefikia asilimia 90.

Kabla ya kueleza mpango huo kulishuhudiwa uendeshaji kesi katika Mahakama ya Watoto( Mahakama Kifani) kwa madereva waliovunja sheria za usalama barabarani kwa kutosimama maeneo yenye alama za watembea kwa miguu yanayotumiwa kuvuka wanafunzi.

Mpango huo umekwenda sambamba na kufadhili mafunzo kwa waendesha bodaboda 300 katika Jiji la Tanga ili kuweza kuzijua sheria za usalama barabarani na namna ya kuweza kuziepuka.

Alisema mara nyingi ajali hizo zimekuwa zikisababishwa na waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda kutokana na baadhi yao kushindwa kufuata sheria za usalama barabarani

Alisema kufuatia uwepo wa changamoto hiyo, Jeshi hilo limendelea kujipanga na kuimarisha usalama hususani kwenye vivuko wavyovukia wanafunzi nyakati za asubuhi wanapovuka ikiwa ni mkakati wa kutokomeza ajali ambazo zimekuwa zikipoteza ndoto zao.

“Kwa kweli sisi kama Mkoa wa Tanga tumejipanga vizuri kuhakikisha tunatokemeza ajali za barabarani hususani kwa watoto na wanafunzi kwa kuhakikisha kila siku hususani nyakati za asubuhi kuna kuwa na askarti wa usalama kwenye vivuto vya watembea kwa miguu kwa lengo kuondosha ajali hizo”Alisema

Alisema watumiaji wa vyombo vya moto wamekuwa wakipuuzia sheria za usalama barabarani licha ya kuzifahamu hivyo ni jukumu la kila mwananchi sasa wahakikishe wanazingatie na kufuata sheria za usalama ili kuweza kupunguza ajali

Awali Meneja wa Shirika la Amend Tanzania Simon Kalolo alisema hilo limetekeleza Mpango Kazi wa Usalama Barabarani kwa Halmashauri ya Jiji la Tanga kwa asilimia 90 huku likitumia nafasi hiyo kueleza hatua mbalimbali za kuutekeleza mpango huo ikiwemo kutoa elimu ya usalama barabarani kwa wanafunzi wa 350 wa shule za msingi.

Alisema Shirika hilo linajishughulisha na usalama barabarani nchini tangu mwaka 2009 na kwa ufadhili wa Shirika la Fondation Botnar jijini Tanga, shirika hilo limekuwa likishirikiana na Halmashauri ya Jiji katika kuboresha miundombinu ya barabara kwenye maeneo ya shule.

“Pia kutoa elimu ya usalama barabarani kwa wanafunzi,kuanzisha klabu za usalama barabarani na mahakama kifani za watoto, mafunzo kwa madereva pikipiki , kuandaa makongamano ya wadau wa usalama barabarani, kufanya tafiti huhusu ajali za barabarani, na kuandaa Mpango Kazi wa usalama barabarani kwa Jiji hilo”Alisema

Akizungumzia Mpango Kazi huo wa usalama barabarani wenye lengo la kuboresha safari salama na endelevu kwa jiji la Tanga alisema ulizinduliwa Novemba 11 ,2022 na tangu ulipozinduliwa kuna mambo kadha yametekelezwa.

Alisema baada ya uzinduzi huo amesema shirika la Amend limefanikia kuzindua miundumbinu katika shule tatu za msingi za Shaaban Robert, Mabawa na Majengo.

“Mpaka sasa tumetoa elimu ya usalama barabarani kwa wanafunzi 3,501 wa shule za msingi Mabawa, Majengo and Shabaan Robert na wengine 3,247 wa shule za sekondari Toledi, Kihere and Kiomoni”Alisema

“Tumeanzisha klabu mbili za shule za usalama barabarani katika Shule ya Msingi Usagara na klabu ya usalama wa baiskeli katika Shule ya Sekondari Usagara, yenye watoto 20 katika kila klabu na tumetoa mafunzo ya usalama barabarani kwa watoto hawa, baada ya kuhitimu kuwa mabalozi, wakipokea vyeti katika hafla ndogo”Alisema

"Shughuli za vilabu hivi zimejumuisha mafunzo, midahalo ya usalama barabarani, michezo, mijadala ya mezani na kushiriki katika kampeni za vyombo vya habari na mafunzo ya msasa kwa madereva wa pikipiki 350 kufanya jumla ya madereva waliopata mafunzo haya kufikia 950."

Kalolo alisema Februari mwaka huu wamesambaza vifaa vya kufundishia usalama barabarani kwa maofisa maendeleo ya jamii katika kata 22 kati ya 27 za Jiji la Tanga.


MWisho.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger