Monday, 7 August 2023

MFUMO WA REEFER CONTAINERS KUNUFAISHA WAKULIMA

...


Kukamilika kwa Mfumo wa Makasha yanayotumia Umeme kwa ajili ya kuhifadhi bidhaa ambazo zinaweza kuharibika kutokana na Joto kutawezesha wakulima mbalimbali wanaotaka kusafirisha bidhaa hizo kwenda nje ya nchi kupitia Bandari ya Tanga Kusafirisha bidhaa hizo bila kuharibika.

Hayo yamesemwa na Afisa Masoko na Huduma kwa Wateja wa bandari ya Tanga Habiba Godigodi wakati wa Maonyesho ya Wakulima Nanenane kanda ya Mashariki Mjini Morogoro ambapo Bandari ya Tanga wanashiriki ili kuweza kutangaza fursa zilizopo.

Habiba alisema kuwa kulikuwa na changamoto kwa Wakulima wanaosafirisha bidhaa kama Matunda mbalimbali pamoja na Maua kushindwa kusafirisha bidhaa hizo kutokana na kutokuwepo kwa njia sahihi ya kuhifadhi bidhaa hizo hivyo bandari ya Tanga imetengeneza  eneo maalum la  kuhifadhia makasha yenye mfumo wa umeme ili waweze kuhifadhi wakati wanapotaka kusafirisha bidhaa hizo.

"Hivyo ni fursa kwenu wafanyabiashara kuitumia Bandari ya Tanga kusafirisha bidhaa hususani wakulima wa matunda mbalimbali pamoja na maua kutokana na uwepo wa sehemu sahihi ya kuhifadhi bidhaa hizo  kupitia makasha yenye mfumo wa umeme "Alisema 


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger