Wednesday, 5 January 2022

TANZANIA YAJIANDAA KUSHIRIKIANA NA BURUNDI KATIKA SEKTA YA USHIRIKA

...

Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika ,Dkt.Benson Ndiege,akifungua Kikao kati ya Tume ya Maendeleo ya ushirika na Balozi wa Tanzania nchini Burundi Dkt.Jilly Malekeo kilichofanyika kwa njia ya mtandao kuhusu ushirikiano wa kiushirika kati ya Tanzania na Burundi leo Januari 5,2022.


Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika ,Dkt.Benson Ndiege,akifafanua jambo wakati wa Kikao kati ya Tume ya Maendeleo ya ushirika na Balozi wa Tanzania nchini Burundi Dkt.Jilly Malekeo kilichofanyika kwa njia ya mtandao kuhusu ushirikiano wa kiushirika kati ya Tanzania na Burundi leo Januari 5,2022.


Mrajis Msaidizi, Masoko na Uwekezaji, Robert Nsunza,akiwasilisha wasilisho la Tume ya maendeleo ya ushirika wakati wa kikao kati ya Tume ya Maendeleo ya ushirika na Balozi wa Tanzania nchini Burundi Dkt.Jilly Malekeo kilichofanyika kwa njia ya mtandao kuhusu ushirikiano wa kiushirika kati ya Tanzania na Burundi leo Januari 5,2022.


Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika ,Dkt.Benson Ndiege,akimsikiliza Balozi wa Tanzania nchini Burundi Dkt.Jilly Maleko (hayupo pichani) wakati akichangia mada wakati wa Kikao kati ya Tume ya Maendeleo ya ushirika na Balozi wa Tanzania nchini Burundi Dkt.Jilly Malekeo kilichofanyika kwa njia ya mtandao kuhusu ushirikiano wa kiushirika kati ya Tanzania na Burundi leo Januari 5,2022.


Baadhi ya washiriki wakifatilia mada mbalimbali wakati wa Kikao kati ya Tume ya Maendeleo ya ushirika na Balozi wa Tanzania nchini Burundi Dkt.Jilly Malekeo kilichofanyika kwa njia ya mtandao kuhusu ushirikiano wa kiushirika kati ya Tanzania na Burundi leo Januari 5,2022.


Naibu Mrajis udhibiti Collins Nyakunga,akichangia mada wakati wa Kikao kati ya Tume ya Maendeleo ya ushirika na Balozi wa Tanzania nchini Burundi Dkt.Jilly Malekeo kilichofanyika kwa njia ya mtandao kuhusu ushirikiano wa kiushirika kati ya Tanzania na Burundi leo Januari 5,2022.

..............................................................................

Na.Alex Sonna,Dodoma

Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania, Dkt. Benson Ndiege, leo Jumatano, 05/01/2022, amefanya Kikao kwa njia ya Mtandao na Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Mheshimiwa Dkt. Jilly Maleko, kuhusu ushirikiano wa kiushirika kati ya Tanzania na Burundi.

Hatua hiyo ni utekelezaji wa Maagizo ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa alipofanya ziara nchini Burundi, Julai 16-17, 2021.

Akizungumza kwenye Kikao hicho, Dkt. Ndiege amesema katika ziara hiyo, Mheshimiwa Rais Samia alielekeza Tanzania na Burundi kubadilishana uzoefu katika Sekta ya Kilimo na Mifugo hususan kwenye uendeshaji wa Vyama vya Ushirika na kuongeza thamani ya mazao ya Kilimo.

“Ni matumaini yangu kupitia kikao hiki tutaweza kujadili vyema maeneo ya ushirikiano katika shughuli za vyama vyetu vya Ushirika na vyama vilivyopo nchini Burundi,” alisema.

Dkt. Ndiege mesema Tume ipo tayari kuhamasisha Vyama vya Ushirika kwenda kubadilishana uzoefu wa Ushirika nchini Burundi na wao kuja kujifunza namna Ushirika unavyofanya kazi nchini Tanzania.

Amebainisha kuwa Tume imekuwa ikifanya kazi ya kuviunganisha vyama hivyo na fursa mbalimbali zikiwepo za masoko na uwekezaji ndani na nje ya nchi.

Awali Mrajis Msaidizi, Masoko na Uwekezaji, Robert Nsunza amesema kuna vyama vya ushirika 9,185 nchini ambapo kati ya hivyo 4,039 ni Vyama vya ushirika wa mazao.

Kwa upande wake, Balozi wa Tanzania nchini Burundi Dkt.Jilly Malekeo, amesema kumekuwapo na changamoto ubalozi unapohamasisha Watanzania kulitumia soko la mchele nchini Burundi kutokana na wanunuzi kuwa kwenye ushirika. Hivyo, changamoto hii inaweza kutatuliwa iwapo kutakuwa na Ushirikiano wa kiushirika kati ya nchi hizo mbili.

“Mtanzania akiingiza mchele Burundi anakutana na uongozi wa Chama cha Ushirika, na anaweza asiuze kwa faida kutokana na kukosa 'connection' nzuri, kwa kuwa wenzetu wana Ushirika kwenye mazao ya nafaka,” amesema Mhe.Balozi Maleko.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger