Monday 3 January 2022

MCHUNGAJI AWAVUA NGUO WANAWAKE ' LIVE' KANISANI..AWAPAKA MAFUTA YA UPAKO WAOLEWE

...
Haya ni maajabu ya fungua mwaka!, ama kweli  basi humu duniani hakuishi vituko kila kuchao. 

 Mchungaji wa kanisa moja nchini Ghana katika mitandao ya kijamii akiwavua nguo wanawake tena kanisani na kuwaogesha na kuwapaka mafuta huku ikidaiwa kwamba kufanya hivyo ni kuwapa upako wa ndoa akina mama hao.

Tukio la aina yake linadaiwa kufanyika siku ya mkesha wa mwaka mpya, Desemba 31, 2021 kuamkia Januari 1, 2022 kaninani hapo ambapo mchungaji huyo ambaye jina lake bado halijafahamika mara moja, amesema kuwa kuwaosha wanawake ni kuwasafisha, kuwaondolea mikosi na kuwapa upako hivyo kuwafanya wawe watakatifu.

Mchungaji huyo raia wa Ghana, amezua mjadala moto mtandaoni kwa kupeperusha video mubashara ya mkesha wa Mwaka Mpya akiwafanyia washirika wa kike tambiko ya kushangaza.

Katika video inayosambaa kama moto mtandaoni, pasta huyo anasikika akiwambia kondoo wake wajitokeze haraka kwa "kuoga takatifu" 

Baadhi ya washirika wanaonekana wakivua nguo zote na kubaki uchi wakiingia ndani ya beseni na baada ya kuogeshwa, pasta mwingine anaonyeshwa akiwapaka mafuta takatifu.

Pasta huyo pia anasikika akisema kuwa licha ya kufahamu kwamba hatua hiyo itazua utata, hana budi ila kuheshimu maagizo ya roho mtakatifu.


 


Pasta azindua chupi zenye picha yake


Huku mtumishi huyo akiwaogesha kondoo wake wa kike, mwingine nchini Nigeria amezindua chupi na sindiria zenye chapa ya picha yake ili kuwasaidia wanawake waseja wanaotamani kuolewa kuwavizia waume zao.

 Kulingana na pasta Dr J.S. Yusuf, ambaye ni mkuu wa Kanisa la Touch for Recovery Outreach International mjini Abuja, aliagizwa na Mungu kuzindua chupi hizo za 'baraka' ili kufungua milango ya ndoa Mwaka Mpya.

Mchungaji huyo alinukuu mstari kwenye kitabu cha Hesabu 23:20 unaosema “Tazama nimepokea amri ya kubariki, naye amebariki, wala siwezi kubadili.” 

Pia alisema kuwa chupi hizo zinapovaliwa na wanawake, zitawasaidia kupigana na magonjwa na kupata bahati njema ya kuwavizia wanaume ambao watawaoa.

 Itakumbukwa kwamba si mara ya kwanza kwa watumishi wa Mungu kufanya mambo ya kiajabu hususan wanaotokea katika mataifa ya magharibi mwa Afrika. 

Mhubiri ambaye ni raia wa Ghana, Osofo Acheampong, alitoa kauli nzito kwa kusema kwamba sio vibaya kwa mwanamume kuwa na mpango wa kando hata ingawa ni mume wa mtu.

Pasta Acheampong, anayesemekana kuwa kiongozi wa Kanisa la Kipentekosti la Sabato, alitoa maoni hayo kwenye mahojiano ya hivi punde huku akitoa mafungu ya Bibilia kuipa uzito kauli yake.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger