Saturday, 4 December 2021

WATU ZAIDI YA 20 WAFARIKI BAADA YA BASI KUTUMBUKIA MTONI

...

Zaidi ya watu 20 wamefariki, 10 wameokolewa baada ya basi kupinduka kwenye mto Mwingi nchini Kenya.

Katika video iliyoonekana na gazeti la Star siku ya Jumamosi, basi hilo lilijaribu kuliongoza gari hilo kupita daraja lililofurika maji kwa usaidizi wa wakazi.


Baada ya dakika chache, basi hilo lilionekana likihangaika kusogeza magurudumu yake kwa vile mawimbi ya maji yalikuwa makali sana hivyo kulipeleka mtoni.


Kamanda wa polisi kaunti ndogo ya Mashariki Joseph Yakan alithibitisha kisa hicho na kuongeza kuwa waumini wa Kanisa Katoliki la Mwingi walikuwa wakielekea harusini.


The Standard limeripoti kuwa basi hilo lilikuwa na takriban watu 30, ajali hiyo ilipotokea saa 11 asubuhi katika Kijiji cha Ngune, Mwingi ya Kati.


Polisi walisema wanakwaya hao walikuwa wakielekea kwenye harusi ya mwenzao.


Baadhi ya abiria walionekana wakipiga kelele na kuinua mikono yao kupitia madirishani huku basi hilo likizama taratibu.

Chanzo - BBC Swahili
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger