Wananchi wakipata huduma ya kupima afya zao wakati wa mradi wa afya kwa jamii uliofadhiliwa na Barrick North Mara
*****
Kampuni ya Madini Barrick kupitia mgodi wake wa North Mara, imefadhili mradi wa kuelimisha wananchi masuala ya afya na kupima magonjwa mbalimbali, kupata chanjo dhidi ya UVIKO-19 pia kujitolea kutoa damu, katika vijiji 11 vinavyozunguka mgodi huo uliopo wilayani Tarime mkoani Mara.
Mradi huo wa wiki 2 ulioanza Septemba 11 na kuhitimishwa Desemba 1,umetekelezwa kupitia Wizara ya Afya chini ya Mganga Mkuu wa wilaya ya Tarime,umewafikia wananchi zaidi ya 3,000 ambao wamejitokeza kupima magonjwa ya UKIMWI, Kifua kikuu, kupata chanjo ya UVIKO-19, na baadhi yao kujitolea kutoa damu kwa ajili ya Benki ya Damu pia wananchi walipata ushauri wa kiafya kuhusiana magonjwa mbalimbali kutoka kwa madaktari waliokuwa wanatekeleza mradi.
Akiongea kwa niaba ya wanakijiji wenzake kuhusiana na mradi huu, Nyamwiga Warioba, mkazi wa kijiji cha Nyamongo,alisema kuwa kupitia mradi huu wananchi wengi wengi wamepata fursa ya kupima afya zao na kupata elimu ya afya kuhusiana na maradhi mbalimbali,ameishukuru Barrick North mara kwa kufanya uwezeshaji unaolenga kuboresha afya za wananchi sambamba na kudhamini maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani.
Kwa upande wake,mkazi wa kijiji cha Matongo,Maria Samweli,amesema yeye pamoja na wanawake wezake wamepata fursa ya kupima magonjwa mbalimbali na kupata ushauri kuhusiana na jinsi ya kukabiliana na magonjwa sugu yanayowasumbua Wanawake wengi na watoto ambapo pia baadhi yao wamepatiwa chanjo ya UVIKO 19.
Naye Julius Sospeter, mkazi wa kijiji cha Nyangoto amesema yeye na wanakijiji wenzake wamehamasika kujitolea kutoa damu kutokana na kupata taarifa kuwa wapo wagonjwa wanaohitaji kuongezewa damu. Aliomba wadau waliofanikisha zoezi hili kuhakikisha linakuwa endelevu na kufanyika mara kwa mara.
Pia aliipongeza Kampuni ya Barrick North Mara kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kuwasogezea wananchi vijijini huduma za afya kwa karibu.
Mganga Mkuu wa Barrick North Mara ,Dk.Nicholas Mboya, aliwashukuru wananchi kwa kuwa na mwamko mkubwa kushiriki zoezi hili la kupimwa afya zao na kupata ushauri wa afya kutoka kwa wataalamu ambalo limepata mafanikio makubwa.Aliishukuru Serikali na taasisi mbalimbali waliszoshirikiana nazo kufanikisha mradi huu ambao umewanufaisha wananchi wengi.
Wananchi wakipata huduma ya kupima afya zao wakati wa mradi wa afya kwa jamii uliofadhiliwa na Barrick North Mara
Zoezi la utoaji huduma ya kupima afya likiendelea
Wananchi wakisubiri kupata huduma ya kupima afya zao wakati wa mradi wa afya kwa jamii uliofadhiliwa na Barrick North Mara
Wananchi wakisubiri kupata huduma ya kupima afya zao wakati wa mradi wa afya kwa jamii uliofadhiliwa na Barrick North Mara
Wananchi wakipata huduma ya kupima afya zao wakati wa mradi wa afya kwa jamii uliofadhiliwa na Barrick North Mara
0 comments:
Post a Comment