Tuesday, 4 August 2020

MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA TANZANIA JAJI MUTUNGI AIONYA CHADEMA

...

Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji mstaafu Francis Mutungi amewaonya CHADEMA kutokana na alichokiita Uvunjifu wa Sheria kwa kuongeza beti la tatu kwenye wimbo wa Taifa.
Mutungi ametoa onyo hilo mara baada ya jana CHADEMA wakati wakiendelea na vikao vya kupitisha jina la  atakaye peperusha bendera ya Chama hicho katika nafasi ya Urais akisema hakutegemea kwa Chama kikongwe Kama CHADEMA kufanya kitendo hicho.

“Kitendo walichofanya sio cha kukaliwa kimya, kilichonisikitisha ni kitendo cha uvunjifu wa Sheria kwa makusudi, kitendo kilichofanyika na CHADEMA ni lile jambo la kuchukua Wimbo wa Taifa na kuongeza aya ya tatu na mbaya zaidi wanasema wanaongeza tuone kinachotokea” Mutungi.

“Rais alionya Wanasiasa wasichokoze Vyombo vya dola, nawakumbusha hakuna Taasisi iliyo juu ya Sheria, kilichofanyika ni kama kunajisi wimbo wa Taifa”,amesema Mutungi.

Amesema kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania na Zanzibar ni kosa huku akivikumbusha vyama vya siasa vyote vinavyoendesha michakato katika vyama vyao kukumbuka kwamba Sheria hazijakwenda likizo.


Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger