Viungo matata wa Klabu ya Manchester United, Paul Pogba (Kulia) na Bruno Fernandes wakipongezaka kwa kazi nzuri.
Klabu ya Wolves imetinga hatua ya robo fainali ya mashindano ya Ulaya kwa mara ya kwanza baada ya takribani miaka 48 baada ya kuibuka na ushindi wa jumla ya bao 2-1 dhidi ya Olimpiacos ya Ugiriki.
Bao pekee lililoivusha Wolves liliwekwa kimiani na mshambuliaji Raul Jimenez aliyefunga kwa penati dakika ya 8 ya mchezo, kufuatia jitihada za Daniel Podence kuzaa matunda baada ya kuangushwa kwenye eneo la hatari na mlinda mlango wa Olimpiacos, Bobby Allain.
Jimenez ambaye ni raia wa Mexico, alifunga bao hilo na kumfanya awe mchezaji pekee wa ligi kuu ya England aliyehusika moja kwa moja katika mabao mengi msimu wa 2019/20 wa mashindano yote, ambaye katika michezo 37,alifunga mabao 27 na pasi zilizozaa mabao 10.
Kwa ushindi huo, Wolves ilisonga mbele kwa jumla ya ushindi wa bao 2-1 na sasa watachuana na itaumana na Sevilla ambayo iliiondosha AS Roma kwa jumla ya mabao 2-0.
Matokeo mengine, Bayer 04 Leverkusen iliifunga Rangers kwa bao 1-0 na kusonga kwa jumla ya bao 4-1na sasa Wajerumani hao watakipiga dhidi ya Inter Milan ya Italia ambayo iliifunga Getafe bao 2-0.
Manchester United ambayo iliifunga bao 2-1 klabu ya LASK katika mchezo wa mwisho, sasa wataumana na FC Copenhagen hatua vilabu vya Shaktar Donetsk watakipiga dhidi ya FC Basel na michezo hiyo itapigwa kuanzia August 10 na 11.
0 comments:
Post a Comment