Karibu vifo vipya 100 vimeripotiwa ndani ya masaa 24 siku ya Jumapili nchini Uturuki, na kusababisha jumla ya vifo vinavyohusiana na ugonjwa wa Covid19 kufikia hadi 1,198 nchini, Waziri wa Afya wa Uturuki, Fahrettin Koca ametangaza.
Mbali na vifo vipya 97, kesi 4,789 mpya za maaambukizi mapya za virusi hivi, ambayo ilitokea nchini China mwezi Desemba kabla ya kusambaa hadi nchi mbalimbali duniani, zilibainika ndani ya siku moja, na kuifanya idadi ya wagonjwa kufikia 56,956 tangu kuanza kwa janaga hilo
Katika juhudi za kupambana na virusi vya Corona, Uturuki kwa mara ya kwanza ilitangaza marufuku ya kutoka nje mwishoni mwa juma lililopita
0 comments:
Post a Comment