Monday, 27 April 2020

SERIKALI YASEMA UHAI WA BINADAMU UNA THAMANI KUBWA KULIKO UHAI WA WANYAMAPORI

...

Serikali imetolea ufafanuzi wa kauli iliyotolewa na  baadhi ya Wananchi  wanaodai kuwa Wizara ya Maliasili na Utalii imekuwa ikithamini uhai wa wanyamapori kuliko uhai wa Binadamu.



 Akizungumza na viongozi wa vijiji vitano vinavyopakana na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti katika wilaya ya Serengeti mkoani Mara, Naibu Waziri Mhe.Constantine Kanyasu amesema  uhai wa binadamu una thamani kubwa na kamwe hauwezi kufananishwa na uhai  wa wanyamapori

Amesema licha ya  kuwa  Binadamu anaaminika kuwa akili kuliko Wanyamapori hata hivyo Wizara hiyo imekuwa ikifanya kila liwezekalo ili kuondoa migogoro kati ya Wanyamapori na binadamu.

" Tunaamini kila binadamu angetamani kuona yupo salama na ndio madhumuni na matamanio ya serikali" Amesisitiza Mhe.Kanyasu.

 Amesisitiza  kuwa  binadamu ana uwezo wa kukwepa mienendo ya wanyamapori na  kuwa katika mazingira salama kuliko mnyama mwenyewe na ameongeza kuwa  wanyamapori hao wapo kwa ajili ya Binadamu na sio vinginevyo.

Akitaja baadhi ya mikakati iliyochukuliwa na Serikali  ili kunusuru uhai wa binadamu ni pamoja na kuhamisha jumla ya Simba 36 kutoka Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na kupelekwa katika Hifadhi nyingine lengo likiwa ni kupunguza madhara kwa binadamu wanaoishi karibu na Hifadhi hiyo.

Amesema jitihada hizo zilizochukuliwa na Serikali kufuatia Simba kula  ng'ombe wapatao  360 kwa kipindi cha mwezi Januari na Februari mwaka huu  huku  baadhi ya Wananchi kuuawa na wengine kujeruhiwa na wanyamapori wakali na waharibifu ni mkakati wa kuona maisha ya binadamu yanakuwa salama.

Licha ya jitihada hizo zilizofanywa na Serikali, Mhe.Kanyasu amewataka wananchi kuchukua tahadhari kwa kujiepusha kulima mazao  pamoja kujenga nyumba karibu na vigingi ili kuepuka athari za wanyamapori hao    kwa vile wanyamapori  wanakapokuja hawajui kuwa wamevuka mpaka.

 Amesema maamuzi hayo ni moja ya jitihada za Serikali kuhakikisha  uhai wa binadamu unalindwa kwa gharama yoyote ile.

Amesema licha ya kuwa moja ya jukumu la msingi la Wizara hiyo ni kulinda na kuendeleza Wanyamapori kwa ajili ya kizazi cha sasa na cha badae lakini hata hivyo thamani ya  Uhai wa binadamu ipo pale pale .


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger