Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka ametuma Salamu za Pole na Rambi rambi kufuatia kifo cha Mwanaharakati wa Haki za Watu Wenye Ualbino Josephat Torner Nkwabi (40) ambaye amefariki dunia baada ya kugongwa na Hiace ‘ Daladala’ akivuka barabara jijini Mwanza.
Kupitia Mtandao wa Instagram, Mhe. Anthony Mtaka ameandika ujumbe ufuatao :
Mungu akupe pumziko la milele kaka na rafiki yangu Josephat Torner Nkwabi,-Ulikuwa mwanaharakati na mdau wa kweli wa maendeleo ya Mkoa wa Simiyu,ajali imekatiza maisha yako,mchango wako kwenye mapambano dhidi ya ukatili wa watu wenye Albino hautasahaulika,uliwasemea,uliwatetea,na zaidi ulijitoa katika kuwatunza na kuwasomesha watoto wenye Albino chini ya Taasisi yako ya "Joseph Torner Foundation" Uliuunganisha mkoa wetu na mashirika mengi ya kitaifa na Kimataifa,wakati wote Simiyu ilikaa moyoni mwako.
Natoa pole kwa familiya yako,mke na wanao,natoa pole nyingi kwa Chama cha watu wenye Albino Tanzania kwa kumpoteza mtu ambaye alijitoa kwa hali na mali kwa faida ya wenzake,zaidi nawapa pole wananchi wa Wilaya ya Busega (Nyumbani)ambao walishirikiana na Josephat katika mambo mengi ya maendeleo.
Hakika hii dunia sisi ni wapitaji,Mungu akupokee kwenye nuru ya uso wake Mbinguni.
0 comments:
Post a Comment