Tetemeko la ardhi limetokea katika Ukanda wa Ziwa Victoria na kuyakumba maeneo ya mikoa ambayo ni jirani na Ziwa hilo ikiwemo eneo la mpaka wa Geita na Shinyanga.
Mjolojia Mwandamizi kutoka taasisi ya Jiolojia Bwana Gabriel Mbogoni amesema Tetemeko hilo lina ukubwa wa 4.6 katika Vipimo vya Richta.
Bwana Mbogoni amesema Tanzania imepitiwa na mkondo wa bonde la ufa la Afrika Mashariki ikiwa na mikondo miwili mkondo wa Mashariki na mkondo wa Magharibi hivyo matukio ya mateteko ya ardhi kwenye mkondo wa bonde la ufa ni lazima yotokee na kuwataka watanzania muda wote wawe kwenye hali ya tahadhari.
Naye Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Geita Mponjoli Lotson amethibitisha kutokea kwa tetemeko katika mkoa wake ambaye amesema Tetemeko hilo limepiga hadi Chato lakini hata hivyo haijasaabisha Madhara.
Mkoani Shinyanga hasa katika Wilaya ya Kahama ambayo inapakana na mkoa wa Geita kupitia kwa Mkuu wa wilaya hiyo Bw. Anna Mringi Macha amethibitisha kutokea kwatuki hilo huku akieleza kuwa pia halijaleta madhara.
Credit:ITV
0 comments:
Post a Comment