Saturday, 25 April 2020

ASIMULIA JINSI ALIVYOKAMATWA BAADA YA 'KUPOST FACEBOOK' KUWA ANA MAAMBUKIZI YA CORONA

...
Michael Lane Brandin aliambiwa kwamba ujumbe wake aliotuma kwenye mtandao wa Facebook utasababisha hisia tofauti.

Kile ambacho hakufahamu ni kwamba atakamatwa, atapoteza kazi na kushtakiwa kwa makosa ambayo huenda yakamfanya akajipata kizimbani.

Ilikuwa ni majira ya mchana mwezi Machi na mjadala kuhusu namna ya kukabiliana na Covid-19 ulipokuwa unaendelea kila mahali.

Hivyo yeye, akaamua kushiriki mjadala huo kwa kuandika.

Michael alituma ujumbe unaosema kwamba yeye amepatikana na virusi vya corona na madaktari walikuwa wamemuambia kuwa virusi hivyo vinaweza kusambazwa kwa njia ya hewa.

Kupitia mtandao wa Facebook, alichokutana nacho hakuamini, kuhurumiwa na mshtuko. Rafiki zangu walimtumia ujumbe kumuuliza kama yuko sawa, na akasema yuko sawa, katika ujumbe wake alikuwa anatania tu,' anasema.

Kipi kilikuwa kinaendelea kando na mtandao hangewahi kukifikiria.

Uvumi tayari ulikuwa umeanza kusambaa kama moto wa msituni katika kaunti yote ya Tyler. Kulingana na polisi katika mji wa Texas, tayari watu walikuwa wameanza kuwa na wasiwasi.

Huo ni wakati ambapo hakuna nchi yoyote ambayo ilikuwa imetoa amri ya kutotoka nje kwa raia wake na pia walikuwa wanapiga simu hospitali uuliza ikiwa taarifa hizo zilikuwa za kweli na kile ambacho wanaweza kufanya kujilinda.
Kibali cha kukamatwa

Polisi ikawasiliana na Michael na kumwambia kwamba arejee kwenye ujumbe wake wa Facebook na kuandika tena kwamba alichokisema hakikikuwa cha kweli na akafanya hivyo.

Hatahivyo, uvumi huo ulikuwa unaendelea kusambaa na ujumbe mwingine katika ukurasa wa Facebook ukawa unatoka kwenye akaunti ya Tyler ofisi ya Sheriff:

'Katika lalamiko rasmi kutoka idara ya makosa ya jinai, hakimu Jacques Blanchett alitoa kibali cha kukamatwa kwa Brandin kwa makosa ya kuzua taharuki kwa taarifa za uwongo.

Brandin akajipeleka kwa mamlaka.

'Nilijipeleka mwenyewe na baada ya mchakato wa kujiandikisha kukamilika, wakasema kwamba usiko huo nitalala jela kwasababu ni lazima nimsubiri hakimu siku itakayofuata.

Nilikuwa na wasiwasi kupita maelezo,' Brandin anasema.

Kwasasa amerejea nyumbani akisubiri siku ya kesi yake kusikizwa ambayo hadi kufikia sasa haijulikani kwasababu ya kusambaa kwa virusi vya coona lakini licha ya kwamba hali ilivyo kwa Brandin bado ni tete, anasema kwamba bado anahisia mchanganyiko kuhusu ikiwa anajutia kile alichofanya au la.Michael Lane Brandin

'Nina shahada ya uanahabari na nimesomea nyanja hiyo kuonesha vile ilivyo rahisi kwa yeote yule kutuma ujumbe mtandaoni na kusababisha wasiwasi.

Pia nilitaka kudhihirisha kwamba ni muhimu kwa watu kuelimika na kufanya utafiti wao kabla ya kukubali kwamba kila wanachokisoma mtandaoni ni cha kweli.

Lakini kwa ujumbe nilioandika Facebook, nimepoteza kazi, mafao yangu ya afya, na pia sikuweza kuanza shahada yangu ya uzamili kwa wakati niliokuwa nimepanga kwa ukosefu wa pesa na hilo limeniongezea mzigo wa kifedha kwa familia yangu kwasababu wote wananisaidia kulipa gharama zangu.

'Licha ya kwamba najutia, nililazimika kuandika barua ya kuacha kazi na kulala jela kwa usku mmoja na pia ama naweza kuambiwa nilipe faini au hata kuhukumiwa kifungo jela. Hayo sio mambo mazuri.'

Katika ofisi ya umma, wamesema wamelazimika kuchukua hatua hiyo kwasababu ya wasiwasi uliokuwa unaendelea kuhusu virusi vya corona Marekani

Marekani sio eneo pekee ambapo ambapo sheria mpya inamaanisha kusambaza taarifa kwa mitandao ya kijamii kuhusu virusi hivyo kunaweza kukufanya ukakamatwa.

Watu waliokamatwa kote duniani

Waliokamatwa kwa kusambaza taarifa za uongo ni taarifa zinazoripotiwa India, Morocco, Thailand, Kenya, Tanzania Cambodia, Somalia, Ethiopia, Singapore, Botswana, Russia na Afrika Kusini.

Katika baadhi ya matukio, uvumi unaweza kusambaa ukiwa na nia njema lakini waangalizi wa haki za Binadamu wametuambia wamesema kwamba wana wasiwasi kuwa janga hili limefanya mafia kuwa na nguvu mno kiasi cha kukandamiza wale wanaowakosoa.
Via BBC Swahili
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger