Na Magnus Mahenge, Dodoma
Mbunge wa Zamani wa Jimbo la Peramiho, mkoani Ruvuma, Dk Damas Mbogoro amefariki dunia katika hospitali ya Peramiho alikokuwa akihudumiwa.
Taarifa ya Spika Job Ndugai iliyosomwa bungeni na Naibu Spika wa Bunge, Dk Ackson Tulia ilisema mbunge huyo wa zamani amefariki jana katika hospitali hiyo. Dk Tulia alisema hayati Dk Mbogoro alikuwa Mbunge wa Peramiho kwa miaka 10 kati ya mwaka 1980-1995 baada ya kumaliza kipindi hicho alichukua jimbo hilo Prof Simon Mbilinyi na sasa lipo chini ya Jenista Mhagama.
Dk Mbogoro pia amewahi kuwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, pia amewahi kuwa mwenyekiti wa Bodi ya Tumbaku nchini. Dk Mbogoro ambaye kitaaluma ni mchumi pia amewahi kuwa Kimishna wa Mipango na Kamishna wa Sensa nchini.
Pia aliwahi kuwa Mwanzilishi wa Taasisi ya Wirima Community ambayo ndiyo chimbuko la Sekondari ya Wirima iliyopo katika eneo la Wino jimboni Peramiho. Baada ya kustaafu, Dk Ndumbaro alikuwa mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT) tawi la Songea.
Hayati Dk Ndumbaro atazikwa leo katika kijiji cha Wino katika Jimbo la Madaba mkoani Ruvuma. Mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi.
0 comments:
Post a Comment