Sunday, 6 October 2019

Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) Lasitisha safari za kwenda Afrika Kusini

...
Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) limesitisha rasmi safari zake kati ya Dar es Salaam na Johanessburg, Afrika Kusini kuanzia Oktoba 7, 2019 na abiria mbao tayari walikuwa wamekata tiketi kuanzia siku hizo watarudishiwa nauli zao.

Taarifa iliyotolewa na ATCL Oktoba 3, 2019 na kusainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Ladislaus Matindi iliwaelekeza mawakala wa tiketi wote kurejesha nauli za wateja hao ambao tayari walikuwa wamekata tiketi.

ATCL ambayo ilikuwa ikifanya safari hiyo mara nne kwa wiki (Jumatatu, Jumatano, Ijumaa na Jumapili) iliacha kufanya safari kati ya miji hiyo Agosti 23,2019 baada ya ndege yake aina ya Airbus A220-300 kuzuiliwa katika uwanja wa Oliver Tambo jiji Johanessburg kwa amri ya mahakama kuu ya Guateng.

Baada ya takribani wiki mbili ndege hiyo iliachiwa huru kwa uamuzi wa mahakama.


Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger