Tuesday, 22 October 2019

Askofu Ezekiel Yona wa kanisa la Morovian Jimbo la Magharibi apiga Marufuku kwa Makasisi wa kanisa hilo kutumia mafuta chumvi na maji katika maombi

...
NA SALVATORY NTANDU
Makasisi na Mashemasi  wa kanisa la morovian jimbo la Magharibi wametakiwa kutojihusisha na vitendo vya  udanganyifu vinavyofanywa na baadhi ya Watoa maombi ambao wamekuwa wakitumia chumvi na maji pamoja na mafuta kuwahadaa waumini wanao hitaji maombi badala yake wafuate maelekezo ya Yesu kristo aliyokuwa akiyatumia katika maombi.

Kauli hiyo imetolewa jana na Askofu wa kanisa la Morovian Ezekiel Yona wa Jimbo la Magharibi katika hafla maalum ya kuliweka wakifu wa jengo jipya la kanisa la moroviani la kahama mjini pamoja na kuwa kuwasimika mashemas 17.

Askofu Yona amewataka Makasisi hao kuepuka maombezi yanayokwenda kinyume na taratibu mungu na badala yake wafuate taratibu na miongozo ya kanisa hilo ambayo ni mafundisho ya kristo ili kuendelea kutangaza habari njema kwa watu wote.

“ Kinachonitatanisha ni kitu kimmoja sasa hivi wapo baadhi ya  watoa huduma za maombi wanaowanywesha mafuta waumini wao na kisha wanaanguka chini na baadae wanawaombea na kuamka,vitendo hivi msivifanye na havikubaliki katika kanisa la Mungu”alisema Askofu Yona.

Katika hatua nyingine Askofu Yona amewataka Makasisi hao kuendelea kuliombea Taifa ili amani iendelee kudumu sambamba na kumwombea Rais John Pombe Magufuli ili aendelee kuwatetea wanyonge sanjari na kurudisha nidhamu serikalini kwa kusimamia rasilimali za nchi.
  
Nao baadhi ya Makasisi wapya waliopewa daraja hilo, Emanuel Sangosango kutoka Kanisa la Morovian kituo cha (SAUTI)Mwanza na Yona Mbogo wa kanisa la Morovian kituo Singida wameahidi kuwa waaminifu katika utoaji wa huduma kwa waumini wao pamoja na kujiepusha na maombi yasiyofuata mafundisho ya Mungu.

Wamesema wapo baadhi ya Wachungaji ambao wanatumia vitu kama vile mafuta, chumvi na maji kuwahadaa waumini wao ili kupona magonjwa mbalimbali waliyonayo jambo ambalo sio la kweli na kutoa rai kwa waumini kuepuka maombi ya namna hiyo.


Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger