Friday 27 May 2016

Majanga ya Mwanza!! Jamaa Apanda kwenye Mnara wa Simu Na Kutaka Kujirusha ili Afe..Aangalia Picha Hapa

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Kijana Mmoja Jijini Mwanza amenusurika kifo baada ya kujirusha kutoka katikati ya mnara wa simu.


Tukio hilo limetokea leo asubuhi na kuvuta hisia za watu wengi waliofika kumshuhudia kijana huo ambaye alipanda katika mnara huo tangu majira ya asubuhi na kukatalia mnarani hadi majira ya saa sita mchana. 




Mashuhuda wa tukio hilo ambao pia ni marafiki wa karibu na kijana huyo, wamesema huenda kijana huyo amefikia maamuzi hayo kutokana na ugumu wa maisha ambao amekuwa akiulalamikia huku wengine wakisema ni kutokana na kuathiriwa na matumizi ya dawa za kulevya ikiwemo gundi ambayo amekuwa akiyatumia. 




Akizungumza kwa niaba ya Kamanda wa jeshi la uokoaji na zima moto mkoani Mwanza, mmoja wa maafisa wa uokoaji Mussa Kaboni, ametoa rai kwa makampuni yenye minara ya simu kuimarisha ulinzi katika minara hiyo ili kuondoa hatari inayoweza kujitokeza kutoka kwa raia wasio wema. 




Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo walionekana kuchukizwa na kitendo cha kijana huyo na kusikika wakifoka kwa hasira na makelele ya hali ya juu "rukaa, ruka sasa, jirushe kama wewe ni mwanaume" hali ambayo ilikuwa ikimuongezea morari kijana huyo na hivyo kujirusha kweli kutoka katikati ya mnara huo. 




Baada ya kijana huyo kujirusha kutoka katikati ya mnara hadi chini, alipoteza fahamu na kukimbizwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza, Sekour Toure kwa ajili ya huduma ya kwanza.

Zoezi la uokoaji lilichukua zaidi ya masaa sita bila mafanikio

Kijana huyo akiwa katika kilele cha mnara huo uliopo barabara ya makongoro-Airpot jijini Mwanza

Kijana akiwa hoi baada ya kujirusha kutoka katikati ya mnara

Kijana akiwahishwa hospitalini huku akiwa hoi baada ya kujirusha kutoka katikati ya mnara


Ghafla kuna jamaa mmoja akatuhumiwa kwa wizi na hapo shughuli nyingine ya kumuokoa na yeye ikaanza upya.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger