Monday, 4 May 2015

NYUMBA 150 ZAVUNJWA NA SERIKALI WILAYA YA ILALA,SASA HAWANA PA KUISHI

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Wakazi wa nyumba zaidi ya mia moja na hamsini zilizokamilika na
zilizo katika ujenzi kwenye eneo la vikongoro -CHANIKA wamejikuta wakipoteza makazi yao baada ya nyumba hizo kuvunjwa na serikali wilaya ya ilala kwa kudaiwa kuwa ni wavamizi.
Ni sehemu ya wakazi wa eneo hilo la vikongoro wakipaza sauti zao mara baada ya ITV kufika eneo la tukio kushuhudia kilichotendeka ambapo wakazi hao wamesema wamevunjiwa nyumba  zao pamoja na zile walizokuwa wakiendelea kujenga ilhali wanamiliki maeneo hayo kihalali.
 
Mmoja kati ya wakazi  wa eneo hilo EFESO MSEMO amesema vijana waliohusika na kufanya  uvunjaji huo walikuwa wakichukua  vitu walivyokuwa wakikuta ndani ya nyumba hizo sambamba na kunywa vinywaji walivyokuwa wakikuta katika maduka wanayoyavunja.
 
Mwenyekiti wa serikali  ya mtaa huo ameiambia ITV kwa njia ya simu kuwa alipewa taarifa na kamanda wa polisi wa wilaya ya kipolisi ya ukonga kuwa uvunjaji huo unatokana na wakazi hao kuvamia katika eneo ambalo linamilikiwa kihalali na mtu mwingine. 

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

TANGAZO LA TOUR MBUGA YA SAADAN

TANGAZO LA TOUR MBUGA YA SAADAN

FUNGUA PAZIA

NDOA ZA UTOTONI

Narudi nyumbani

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger