Monday 4 May 2015

MPYA:'MAMA ATUPA MTOTO ,KISA UGOMVI WA KIMAPENZI"

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Binadamu wamepoteza utu! Mwanamke mjamzito aliyefahamika kwa jina la mama Janeth, mkazi wa Kimara-Suka jijini Dar anadaiwa kujifungua kisha kukiweka kichanga kwenye begi
na kukitupa shambani, kisa kikielezwa kuwa ni mgogoro wa kimapenzi na mwanaume aliyempa ujauzito.
Mama anadaiwa kutupa kichanga hicho akijaribu kuangalia huku na kule kama kuna mtu anamuona alifahamika kwa jina la mama Janeth.
Mmoja wa mashuhuda akizungumza na gazeti hili, alisema kichanga hicho kilikutwa na bibi  anayejulikana kwa jina la mama Joyce katika shamba lake lililopo eneo la Moa, Kimara-Suka baada ya kubanwa sana mama Janeth alikiri kuwa ndiye mwenye kichanga hicho.
Msamaria mwema akiangalia mfuko uliotupwa ukiwa na mtoto ndani.
Kufuatia kuulizana ndipo mwenye shamba akakumbuka kuwa mama Janeth alikuwa mjamzito na ilionekana alijifungua usiku,  walipombana sana alikubali kukitupa kichanga hicho.
Picha ya mtoto huyo alietupwa na mama yake aliefahamika kwa jiana la mama Janeth.
Ijumaa Wikienda lilizungumza na mmoja wa mashuhuda ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema kuwa mama huyo alipohojiwa alisema mwanaume aliyempa ujauzito aliukataa ndipo akaamua kufanya kitendo hicho.
Wananchi walifanikiwa kumtia mikononi mama Janeth na kumhoji ila wakiwa wanajianda kuwaita polisi, mwanamke huyo alichoropoka kiaina na kwenda kusikojulikana.
Baada ya polisi kufika eneo la tukio, mama Janeth alikuwa kishatoroka na polisi wakalazimika kuwachukua baadhi ya majirani kwa ajili ya mahojiano zaidi, huku mwili wa kichanga hicho ukipelekwa kuhifadhiwa Hospitali ya Tumbi, Kibaha.
“Wanawake mnapaswa kuwa makini sana katika suala la uhusiano kwani mnapokosea ndiyo chanzo cha kupata ujauzito na mwisho mnawatupa watoto wenu, ” alishauri shuhuda huyo ambaye hakupenda jina lake liwe wazi.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger