Monday 4 May 2015

TAARIFA KAMILI KUHUSU KUPANDA KWA (PESA YA CHAKULA) BOOM KWA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU 2015

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
                       
Baada ya kupost habari hiyo kuhusu kupanda kwa boom la wanafunzi wa elimu ya juu ,wanafunzi na watu wengi wamekuwa
na shauku ya kutaka kujua ukweli kamili wa taarifa  hii na wengine wakisema  kuwa hakuna kitu kama hichi na wala hakiwezi kutokea.

Maswayetu Blog tumeweza na tumethubutu kufuatilia hadi ofisi za bodi ya mikopo na kukutana na mfanyakazi mmoja na ametuambia kuwa  ni kweli pesa imeongezwa hiyo ni kutokana na gharama za maisha kupanda,hivyo basi baada ya kulijua hilo wameamua kuiongeza hadi tshs.8500 kutoka tshs.7500.

Pia tulimuuliza swali kwamba hawaoni kwamba pesa hii bado itakuwa ndogo sana kwani wanafunzi wali demand tshs 10000 na si 8500,alisema kwamba wamefanya tathmini na kugundua kwamba pesa hii itatosha wanafunzi wengi wanataka tshs.10000 mostlly wanataka kupata pesa ya ziada ya kufanya starehe wakati katika pesa tunayowapatia hilo halipo.

Tafadhali toa maoni yako hapo chini,je umeridhika na upandaji wa pesa hii?,
 waweza kuchati na blogger kwa kumtumia email kwenda inocentlugano60@gmail.com.

Waweza kusoma taarifa hii wewe mwenyewe kwa kutembelea hapa www.heslb.go.tz.

BONYEZA HAPO CHINI KUWEZA KUPATA TAARIFA MBALIMBALI
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger