Tuesday 5 May 2015

Mgomo wa Madereva: Milio ya Risasi na Mabomu Yarindima Stendi Kuu ya Mabasi Ubungo Dar

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY


Jeshi la Polisi limelazimika kutumia mabomu ya machozi leo asubuhi katika kituo cha mabasi ubungo jijini Dar es Salaam baada ya madereva ambao wanaendesha mgomo kuanza kuwarushia mawe baadhi ya viongozi waliofika kwa ajili ya mazungumzo na madereva hao akiwemo mkuu wa wilaya ya Kinondoni Bw. Paul Makonda na mkuu wa kikosi cha usalama Barabarani, DCP Mohamed Mpinga.

Akiongea na mtandao  huu, Afisa kutoka chama cha kutetea abiria, CHAKUA, bw, Gervas Lutaguzinda amesema kuwa madereva walianza kuwarushia mawe viongozi hao baada kudai kuwa ahadi wanazozitoa sio za msingi hivyo kutaka waziri mkuu afike eneo hilo.

Hata Hivyo Bw Lutaguzinda amesema kuwa hali kwa sasa imetulia na viongozi hao wanaendelea na mazungumzo na madereva hao ili kufikia muafaka wa tatizo hilo ambalo limefanya baadhi ya abiria kulala kwenye magari tangu jana.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger