Monday 4 May 2015

MVUA ILIYONYESHA KWA MASAA MAWILI YABOMOA NYUMBA 80 HUKO KITETE,

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Nyumba kadhaa zimeboka  na nyingine   80  kujaa maji  kufuatia
 mvua kubwa iliyonyesha kwa masaa mawili katika vijiji vya kitete na kadudu wilaya ya kilosa mkoani morogoro na kusababisha uharibifu wa  mazao   na baadhi ya familia kukosa makazi.
Wakizungumza kwa huzuni wananachi wa vijiji vya kitete na kadudu wameeleza mvua  zimesababisha  madhara  makubwa ikiwemo nyumba kuanguka na kusababisha  baadhi ya kaya  kukosa makazi  ambapo  kwa sasa wananchi hawana chakula kutokana na vyakula kuharibika baada ya kujaa maji   huku mazao yaliopandwa mashambani yakiwemo mahindi  yameseombwa na mvua   na kuomba serikali kuwasaidia  chakula  wanachi waliokubwa na  mafuriko.
 
Akitoa tarifa za tathmini ya awali ya mafuriko hayo afisa tarafa wa tarafa ya dumila  MOSES NCHIMBI amesema  nyumba zilizo anguka kabisa ni nane  na nyingine 80 zimeharibika  vibaya na kujaa maji  ambapo ameeleza chanzo cha athari hizo  hayo ni kuziba kwa  mto DYONGOYA  kutokana na baadhi ya wananchi kulima kando ya mto huo.
 
Mkuu wa wilaya ya kilosa BWANA JOHN NJEWELE amewapa pole wananchi wa vijiji hivyo kwa athari walizozipata  ambapo ameagiza watendaji wa vijiji kata na vitongoji kuanza zoezi la kukagua  na kubaini  wananchi waliolima  na kujenga kando kando  ya mito  na kusabaisha mito kuziba na maji kupoteza uelekeo na kujaa katika makazi  ya wananchi.
 

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger