Wednesday 13 December 2023

ZAIDI YA WATU 233,000 KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI WA MUGANGO- KIABAKARI-BUTIAMA

...

Naibu wa Waziri wa Maji Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) amewataka wakandarasi wa mradi wa maji wa Mugango- Kiabakari-Butiama waweze kukamilisha utekelezaji wa Ujenzi wa mradi huo ili wananchi zaidi ya laki 233,000 waweze kunufaika na huduma ya upatikanaji wa majisafi na salama.

Mhandisi Mahundi ameyasema hayo Disemba 11 Wilayani Butiama Mkoani Mara wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa ujenzi wa Mradi wa maji wa Mugango-Kiabakari- Butiama na Mradi wa Maji wa Kijiji cha Kyankoma-Kiagata.

Katika ziara hiyo, Mhe. Mahundi amewasisitiza Wakandarasi hao waweze kukamilisha utekelezaji wa Ujenzi wa Mradi wa hiyo ili wananchi wapate huduma ya maji safi na salama.

"Mwishoni mwa mwezi Disemba, 2023 Mradi huu, uwe umekamilika kulingana na mkataba wa nyongeza. Pia, namuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mugango/Kiabakari kuweza kusimamia utekelezaji wa mradi huu"amesema Mhandisi Mahundi

Kadhalika Mhandisi Mahundi amezindua Mradi wa Maji wa Kijiji cha Kyankoma-Kiagata ambao umetekelezwa na fedha za P for R kwa gharama ya shilingi Million 609.2. ambapo inaelezwa kuwa kukamilika kwa mradi huo utaweza kunufaisha wakazi wapatao zaidi ya elfu 5,200.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Butiama Mheshimiwa Jumanne Sagini ambaye ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ameishukru Serikali kwa utekelezaji wa Ujenzi wa Mradi wa Maji wa Mugango – Kiabakari – Butiama ambao unatumia chanzo cha maji cha uhakika cha ziwa Victoria akisema kukamilika kwa mradi huo kutapunguza kero ya ukosefu wa maji katika eneo hilo.




Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger