Monday, 6 February 2023

SBT NA TEMDO WABUNI MITAMBO YA KISASA YA SUKARI ITAKAYO MSAIDIA MKULIMA KUONGEZA THAMANI YA MAZAO YA MIWA

...









Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Antony Mavunde akitoa maelekezo Kwa Mkurugenzi Mkuu wa TEMDO muhandisi Prof. Frederick Kahimba alipo tembelea Shirika la Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO)lililopo ndani ya halmashauri ya jiji la Arusha








Mkurugenzi Mkuu wa TEMDO muhandosi Prof. Frederick Kahimba akitoa maelezo ya Mtambo wa Kuzalisha Sukari ulio Buniwa na Kutengenezwa na TEMDO kwa Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Antony Mavunde alipo tembelea Shirika la Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO)Waziri aliambatana na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Tanzania Prof. Kenneth Bengus


Na Woinde Shizza , ARUSHA

Bodi ya sukari (SBT)inashirikiana na wadau wa maendeleo wakiwemo taasisi ya uhandisi na usanifu mitambo (TEMDO) ilikuboresha kuboresha na kubuni mitambo ya kisasa ya kuzalisha sukari kwa wingi itakayowezesha wakulima na wafanyabiashara kuanzisha viwanda vya kuzalisha sukari hapa nchini.


Sekta ya viwanda nchini ni kiungo muhimu katika ukuzaji wa uchumi wa taifa hali ambayo iliyopelekea Naibu Waziri wa Kilimo Antony Mavunde kufanya ziara katika taasisi ya ubunifu na usanifu mitambo (TEMDO)na kuona ubunifu wa mitambo ya kilimo itakayokuza biashara ya sukari hapa nchini.


Akiongea katika ziara hiyo Naibu waziri huyo alisema kuwa ni lazima tutengeneze mashine au viwanda ambavyovitasaidia wakulima kuongeza thamani katika mazao yao.


"Lazima tufikie katika kuongeza thamani na nyinyi mliopo chini ya wizara ya viwanda , biashara na uwekezaji mhakikishe mnafanya kazi ya kutengeneza mitambo ya kuongeza thamani na hasa katika mazao ya kilimo ,uvuvi pamoja na mifugo mmepewa jukumu kubwa kama temdo na mimi ningependa kila siku muendelee kuja na bunifu mbalimbali", alisema.


Alisema kuwa wanaamini mitambo hii ikikamilika kwa muda muaafaka kama walivyomuaidi hadi kufika mwezi Junu itasaidia kumtoa mkulima katika ukulima wa miwa na kwenda kuwa mzalishaji wa sukari.


"Niwaombe muendelee kuboresha huduma mnayo nafasi kubwa ya kuwasaidia wananchi ,pia nimpongeze mkurugenzi wa bodi ya sukari kwa bunifu walioufanya na kuamua kushirkiana na TEMDO mlikaa na kutafuta jinsi ya kumsaidia mkulima kuondoka na tatizo la miwa kubaki shambani na kuharibuka ,kuna kipindi uwezo wa uchakataji wa miwa katika viwanda vikubwa uliwaliwazidi nakuanza kutokuchukuwa miwa ya wakulima ,bodi iliamua kuchukua hatua kwamba huyu mkulima aliyekwenda shambani akaweka muda wake akatumia gharama leo miwa yake inaozea shambani hali ambayo ilikuwa inawavunja moyo wakulima ,lakini pia kama nchi tulikuwa tunajipunguzia mapato lakini pia tulikuwa tunawafanya watu wachukie kilimo hivyo Mtambo wa Kuzalisha Sukari utamuokoa mkulima .


Alibainisha kuwa mtambo huu utasaidia kuongeza dhamani ya mazao ya kilimo kwa yule mkulima ambaye analima miwa na yupo sehemu ambayo awezi kupeleka miwa yake katika kiwanda kikubwa na utasaidia kukuza uchumi wetu wa nchi yetu ,na alisisitiza kuwa lazima taasisi hizo zijikite katika kutengeneza mitambo itakayosaidia kuongeza thamani katika mazao ya Kilimo ,Mifugo na Uvuvi.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa bodi ya sukari Prof. Keneth Bengesi alisema kuwa lengo la kutengeneza mashine hii ni kuhakikisha wanamsaidia mkulima pamoja na kuhakikisha kwamba hawauzi mazao ya miwa ambayo hayajaongezewa dhamani maana mkulima anapoongeza thamani mazao yake anapata pesa nyingi zaidi.



Mkurugenzi wa taasisi ya ubunifu na usanifu mitambo (TEMDO) Mhandisi Prof. Frederick Kahimba alisema wameshaanza kutengeneza mitambo mbalimbali itakayomsaidia mwananchi na kuhakikisha yale matatizo ambayo yapo katika wizara ya kilimo wao kama Taasisi ya usanifu wanayatatua na kufanyia kazi.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger