Monday, 21 December 2020

Waziri Aweso Afanya Ziara Ya Kushtukiza Usiku Kukagua Mradi Wa Maji Mzakwe Dodoma.

...


Na Faustine Gimu

Waziri wa Maji Jumaa Aweso  ameridhishwa na utekelezaji wa mradi wa maji wa Mzakwe wenye thamani ya zaidi ya milioni 200 unaotarajiwa kupunguza adha ya maji kwa mkoa wa Dodoma huku akimuagiza Katibu Mkuu wa wizara hiyo kuhakikisha vinachimbwa visima vingine vikubwa viwili .

 Waziri Aweso ameyasema hayo usiku wa Disemba 20,2020 wakati akizungumza na waandishi wa habari alipofanya ziara ya kushtukiza kukagua utekelezaji wa mradi wa maji wa Mzakwe ambapo amesema Wizara imeipatia Bilioni Moja Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dodoma(DUWASA) kutatua changamoto hiyo.

 Amesema adha ya maji imetokana na kuwepo kwa ongezeko kubwa la watu akisema kuwa kwa uhitaji wa maji mkoa wa Dodoma ni lita milioni 103 wakati uzalishaji wa sasa ni lita milioni 66 ikionyesha upungufu wa lita milioni 37 huku akibainisha kuwa kisima hicho kinatarajiwa kuzalisha lita laki nne kwa saa.

  Pia Waziri Aweso ametoa onyo kwa baadhi ya watu wanaofanya mgao wa maji bila kufuata utaratibu  akisema wizara haitomvumilia yeyote anatakayebainika  kufanya ubabaishaji kwani serikali imejipanga kufanya kazi usiku na mchana  kufikisha kwa kila mtanzania huduma hiyo.

 Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji  DUWASA ,Mhandisi, Aron Joseph amesema mradi huo unafanywa na Kampuni ya Shanxi akieleza kuwa kisima kitakuwa na urefu wa mita 150 ambapo hadi sasa kimefikia theluthi ya utekelezaji wake mradi huo ulitarajiwa kukamilika ndani ya siku 60 lakini watatekeleza kwa muda wa siku 30.

Aidha Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi, Anthony Sanga akaahidi kutekeleza maagizo yaliyotolewa huku akiwahimiza watanzania kuendelea kutunza vyanzo vya maji katika maeneo yao
.


 



Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger