Sunday, 13 December 2020

MAHAFALI YA 14 YA CHUO KIKUU ARDHI WASICHANA WAZIDI KUN'GARA

...

Mlau akiwa amebeba kitabu na mesi akiwa pamoja na wahadhiri kwenye andamano la wanataaluma kutokea jengo la utawala kuelekea kwenye viwanja vya chuo hicho kushiriki mahafali ya 14 chuoni hapo Disemba 12 2020.

Na Robert Okanda - Dar es salaam
Wanafunzi wa kike wameendelea kutia fora kwa kufanya vizuri katika masomo yao katika Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Hayo yamebainishwa jijini Dar es Salaam jana katika mahafali ya 14 ya Chuo hicho yaliyohudhurishwa na Mkuu wa Chuo hicho, Waziri Mkuu Mstaafu David Cleopa Msuya.

Kwa mujibu wa Makamu Mkuu wa ARU, Profesa Evaristo Liwa wahitimu 926 wamepeta digrii zao baada ya kuhudhuria masomo na kutunukiwa shahada mbalimbali, ambapo chuo hicho utoa shahada za uzamivu, shahada za uzamiri na shahada ya kwanza.

Amesema kulikuwa na asilimia 43 ya wanawake jambo ambalo linawapa furaha sana kwa sababu asilimia 43 ya wafanyakazi wa chuo hicho ni wanawake pia ikimaanisha asilimia 100 ya waliofanikiwa kumaliza masomo yao, na sio wanaume.

Wanawake wanafanya vizuri sana, hata kwenye hafla ya kuwatunuku wanafunzi waliofanya vizuri kwenye masomo yao, mwanafunzi bora kuliko wote kati ya 87 miongoni mwao 44 walikuwa wanaume, 43 walikuwa wanawake. Asilimia 49 ya wanawake wote waliopewa zawadi zao baada ya kufanya vizuri kwenye masomo yao. 

Sio hivyo tu aliyefanya vizuri kuliko wote kabisa kwa mwaka huu ARU alikuwa Yasmin Mnndeme na ameelezea kufarijika sana. Siri ya mafanikio kwa wananfunzi wa kike ni nidhamu. 

"Kinachowafanya wanafunzi wa kike wafanye vizuri zaidi ni nidhamu na kuwa wasikivu kufuatilia yale ambayo wanayosema wahadhiri na kutojihusisha na kuzurura zurura", alifafanua Profesa Liwa.

Makamu Mkuu huyo ametoa wito kwa wanawake waliokuwa na woga wa kusoma masomo hayo kujiunga na chuo hicho ili wasaidiwe kufikia malengo yao ya kulitumikia taifa baada ya kupata maarifa katika fani mbalimbali zitolewazo na chuo hicho.

Akaongeza kwamba kwa miaka miwili mfululizo wamekwenda Jeshi la kujenga taifa (JKT) na wamefanikiwa kupata wananfunzi wengi ambapo idadi ya wanawake wanaojiunga na chuo imeongezeka kutoka asilimia 34 hadi 44.

Amewatoa hofu kupuuza ile dhana ya zamani kwamba masomo ya maswala ya ardhi ni ya wanaume aipo tena, wanawake kwa sasa wanafanya vizuri kwenye fani mbalimbali na ni jukumu la chuo pia kuwapa ujasiri ili wajiunge na kufanya vizuri kwani hata baadhi ya programu ni za wanawake.

Alihitimisha kwa kuwakumbusha wanawake kwamba taaluma walizohitimu ni nyeti sana kwani taaluma hizo ndizo zinazohitajika sana kuliko kipindi kingine chochote kwa sababu Taifa letu tunatoka kwenye uchumi wa kati kwenda kwenye uchumi wa viwanda.
Amesema kwa sasa wao ndio wanaohitajika. Wajenzi, wathamini, watu wa mazingira wote wanatoka chuoni hapo, wajue wanao umuhimu mkubwa sana.

Serikali imejipanga kuwatumia wataalam wazalendo na inataka kutumia wataalam wake wazalendo. Amesema chuo kinaona fahari kuwa na wataalam wake wenyewe na sio wa kutoka nje.
Brass bendi ikitumbuiza katika hafla ya mahafali hayo. Picha zote na Robert Okanda
Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Waziri Mkuu mstaafu Cleopa David Msuya akimtunuku Mulengeki Editha Felician Shahada ya Uzamivu ya Chuo Kikuu Ardhi wakati wa mahafali ya Kumi na Nne chuoni hapo jijini Dar es Salaam, Disemba 12 2020. Kulia kwake ni Mkamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Evaristo Liwa na waadhiri waandamizi.
Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Waziri Mkuu mstaafu Cleopa David Msuya akiongoza mhadhara kuimba wimbo wa Taifa wakati alipokwenda kuhudhurisha mahafali ya Kumi na Nne chuoni hapo jijini Dar es Salaam, Desemba 12 2020. Kulia kwake ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Evaristo Liwa, Mwenyekiti wa Baraza la Chuo hicho, Profesa Costa Mahalu (kushoto kwake) na viongozi waandamizi wa ARU.
Sehemu ya wahitimu wakijipongeza baada ya kuhitimu katika fani mbalimbali za elimu chuoni hapo.
Sehemu ya wageni wakifuatilia matukio ya hafla ya mahafali hayo.
Sehemu ya wahitimu wakihudhuria mahafali ya kuhitimu katika fani mbalimbali za elimu chuoni hapo.
Sehemu ya wahitimu wakijipiga selfie baada ya kumalizika kwa hafla ya mahafali hayo.
Sehemu ya wahitimu wakijipiga selfie baada ya kumalizika kwa hafla ya mahafali hayo. 
Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Waziri Mkuu mstaafu Cleopa David Msuya akiwa katika picha ya pamoja na waadhiri na viongozi mbalimbali wa chuo hicho wakati wa kuhitimisha mahafali ya 14 chuoni hapo jijini Dar es Salaam, Disemba 12 2020. Pamoja nao (wa pili kulia) ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Tekinolojia Profesa James Mdoe. 

Picha zote na Robert Okanda
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger